Kikosi cha Yanga kinaondoka leo jijini Mbeya kuelekea Morogoro kwa ajili ya mchezo wa ligi dhidi ya Mtibwa Sugar FC.

Yanga inaondoka jijini humo baada ya kukubali kufungwa jumla ya mabao 2-0 dhidi ya Tanzania Prisons jioni ya jana na kuzima rasmi ndoto za kuutetea ubingwa wa ligi.

Kikosi hicho ambacho kina wachezaji wengi wa timu B, kitakuwa na kibarua kingine kigumu dhidi ya Mtibwa Sugar katika Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro Mei 13 2018.

Mtibwa wametamba kufanya vizuri kuelekea mechi hiyo ambapo sasa wanaendelea na mazoezi wakiisubiri Yanga.

Kupoteza kwa Yanga jana kumeifanya Simba iwe bingwa rasmi wa Ligi Kuu yenye alama 65 ambazo haziwezi kufikiwa na timu yoyote ile na ikiwa imebakiza michezo mitatu kukamilisha ratiba6
Share To:

msumbanews

Post A Comment: