Ikiwa Ligi nyingi za mpira wa miguu duniani zinaelekea kumalizika kwa msimu wa mwaka 2017/18 tayari orodha ya wachezaji 20 wa mpira wa miguu walioingiza mkwanja mrefu imeshatoka. Na kwenye orodha hiyo jambo la kushangaza ni kwamba EPL inayotajwa kuwa ligi yenye thamani kubwa duniani na inayotumia pesa nyingi kwenye usajili imetoa majina ya wachezaji wawili pekee, hii ni kwa mujibu wa mtandao wa France Football .
Picha inayohusiana
Lionel Messi
Kwa mwaka huu aliyeongoza orodha hiyo ni mshambuliaji wa klabu ya Barcelona, Lionel Messi ambaye yeye ameingiza kiasi cha Euro milioni £110.2 akifuatiwa na Cristiano Ronaldo £82.2 ambaye kwa miaka miwili mfululizo ameongoza orodha hiyo .
Tokeo la picha la ronaldo
Cristiano Ronaldo
Neymar Jr na Gareth Bale hao wameshika nafasi ya tatu na ya nne kwa kuingiza kiasi cha Euro Milioni £71.3 na £38.5 kila mmoja.
Tokeo la picha la neymar
Neymar Jr
Ligi Kuu ya Uingereza (EPL) kwenye orodha hiyo imetoa majina mawili pekee, Paul Pogba na Alexis Sanchez wote kutoka klabu ya Manchester United na wameingiza kiasi cha Euro milioni £19.2 na £20.6 huku La Liga ikiingiza majina 10 kwenye orodha hiyo.
Tokeo la picha la alexis sanchez
Alexis Sanchez
Vigezo vinavyotumika katika orodha hiyo ni majumuisho ya mishahara na bonasi za wachezaji pamoja na fedha wanazoingiza kupitia matangazo.
TAZAMA ORODHA KAMILI HAPA CHINI KUANZIA WA 20 HADI NAMBA 1:
20) Manuel Neuer (Bayern Munich): £18.2m a year.
19) Paul Pogba (Manchester United): £19.2m
18) Robert Lewandowski (Bayern Munich): £19.4m
17) Oscar (Shanghai SIPG): £19.4m
16) Edinson Cavani (PSG): £19.7m
15) Thomas Muller (Bayern Munich): £20.1m
14) Karim Benzema (Real Madrid): £20.6m
13) Alexis Sanchez (Manchester United): £20.6m
12) Ezequiel Lavezzi (Hebei China Fortune): £22.1m
11) Andres Iniesta (Barcelona): £22.3m
10) Luis Suarez (Barcelona): £22.7m
9) Antoine Griezmann (Atletico Madrid): £22.7m
8) Zlatan Ibrahimovic (LA Galaxy): £23.4m
7) Sergio Ramos (Real Madrid): £24.1m
6) Toni Kroos (Real Madrid): £24.7m
5) Gerard Pique (Barcelona): £25.4m
4) Gareth Bale (Real Madrid): £38.5m
3) Neymar (PSG): £71.3m
2) Ronaldo (Real Madrid): £82.2m
1) Lionel Messi (Barcelona): £110.2m
Share To:

msumbanews

Post A Comment: