Wizara
 ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kupitia Ubalozi wa 
Tanzania nchini Ufaransa kwa kushirikiana na Taasisi ya Sekta Binafsi 
Tanzania (TPSF), inaratibu ziara ya viongozi wa makampuni ya biashara 
zaidi ya 30 kutoka Ufaransa ambao ni wanachama wa Taasisi ya Sekta 
Binafsi ya Ufaransa (MEDEF) yenye mtandao wa makampuni zaidi ya 7100..
Ziara
 hiyo itakayofanyika kuanzia tarehe 15 – 18 Aprili 2018, inalenga kukuza
 ushirikiano wa biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na Ufaransa; 
kutangaza fursa mbalimbali za uwekezaji zilizopo nchini Tanzania; 
kushawishi makampuni makubwa ya Ufaransa kuwekeza Tanzania katika sekta 
mbalimbali zikiwemo nishati, miundombinu, viwanda, maji n.k na kutoa 
fursa kwa wafanyabiashara kutoka Tanzania na Ufaransa kubadilishana 
uzoefu na kuanzisha ushirikiano baina yao.
Ukiwa
 nchini, ujumbe huo utapata fursa ya kufanya mazungumzo na viongozi 
wakuu wa serikali na kushiriki katika Kongamano la Biashara na Uwekezaji
 baina ya Tanzania na Ufaransa litakalofanyika tarehe 18 Aprili 2018, 
jijini Dar es Salaam.
Aidha,
 baada ya kongamano hilo, Wizara kupitia Ubalozi wa Tanzania nchini 
Ufaransa kwa kushirikiana na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania 
(TANTRADE) itafanya mkutano na wafanyabiashara Wakitanzania wenye nia ya
 kutafuta masoko nchini Ufaransa, tarehe 20 Aprili 2018. Ubalozi 
utaelezea fursa zilizopo nchini Ufaransa na mikakati ya kufanya bidhaa 
za Tanzania hususan za kilimo ziweze kuuzwa nchini humo.
Wizara inatoa wito kwa Wafanyabishara wa Tanzania kushiriki kikamilifu na kuchangamkia fursa hii muhimu.

Post A Comment: