Video queen maarufu nchini, Agnes Gerald ‘Masogange’ amefariki dunia hivi punde (leo Aprili 20, 2018) katika Kituo cha Huduma za Afya cha Mama Ngoma, Mwenge jijini Dar es Salaam baada kuzidiwa ghafla jana na kukimbizwa hospitalini hapo. 

Taarifa ambazo hazijathibitishwa, zinadai Masogange alifikishwa Hospitalini hapo akisumbuliwa na homa ya matumbo na tatizo la kupungukiwa na damu.Bloh hii  imefika hospitalini hapo na kujionea umati wa watu waliokusanyika wakilia kwa uchungu kumpoteza msanii huyo.

Dkt. Kihama Ngoma amethibitishia na kusema taarifa zaidi zitatolewa baadaye.

Tayari mwili wa marehemu Masogange umehamishwa hospitalini hapo na kupelekwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa ajili ya kuhifadhiwa.

Mpendwa msomaji wetu, tunakukumbusha Kuidownload Application yetu ya MsumbaNews ili upate habari zetu kwa wepesi zaidi kama vile Magazeti kuliko ilivyo sasa.



Tumekurahisishia; 


Share To:

msumbanews

Post A Comment: