Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI Selamani Jafo  akitoa maelekezo alipokuwa akikahua ujenzi unaoendelea wa Kituo cha Afya Usariver mkoani Arusha.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI Selamani Jafo  akitoa maelekezo alipokuwa akikahua ujenzi unaoendelea wa Kituo cha Afya Usariver mkoani Arusha.
Wataalam wa Afya wa Kituo cha Afya Usariver mkoani Arusha wakiwa katika picha na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI Selamani Jafo huku wakionesha furaha yao baada ya kujengewa majengo mapya.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI Selamani Jafo akipokea taarifa kutoka kwa wataalam wa ujenzi wa Kituo cha Afya Usariver mkoani Arusha.
Moja ya majengo mapya yanayojengwa kituo cha Afya Usariver mkoani Arusha.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI Selamani Jafo akikagua maeneo mbalimbali ya ukarabati wa kituo cha Afya Usariver mkoani Arusha unaoendelea.


Wananchi wilayani Arumeru Mkoani Arusha wamempongeza Rais John Magufuli kwa wema wake katika kuwajali wananchi.

Pongezi hizo zimetolewa mbele ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI Mhe. Selemani Jafo wakati akikagua ujenzi unaoendelea katika Kituo cha Afya cha Usa river kinachoboresha kwa kukijengea jengo la upasuaji, wodi ya wazazi, maabara, nyumba ya daktari na maboresho mengine ya majengo ya kituo hicho.

Katika ziara hiyo, wananchi walionyesha furaha yao kwa kumshukuru Rais Magufuli kwa kuwa ameonyesha kuwajali sana kwa kuwafanyia maendeleo makubwa sana katika kituo cha cha afya. 

Akizungumza katika ukaguzi huo, Waziri Jafo amewataka wananchi wa Arumeru kuendelea kushirikiana na serikali kwa hali na mali kwa ajili ya maendeleo yao na Tanzania kwa ujumla.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: