Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limamshikilia Selemani Masoud (60) mkazi wa Yombo Kialakala kwa tuhuma za kutengeneza vyeti vya kugushi vya vyuo na taasisi mbali mbali za za serikali, nyaraka za serikali na mihuri bandia.

Hayo yamesemwa leo, Ijumaa, Machi 16, 2018 na Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar, Lazaro Mambosasa wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini humo.

“Baada ya kupata taarifa kutoka kwa chanzo chetu, tulimkamata mtuhumiwa na kufanya upekuzi nyumbani kwake, tulikuta nyaraka mbalimbali na jumla ya mihuli 53, nyaraka za Necta, mihuli ya Veta, UDSM, Chuo cha Bandari, Chuo Kikuu Huria cha Tanzania, SUA, Mtwara Universirty, Mkuu wa Chuo Cha UDSM, TRA, NIT, IFM, Bodi ya Taifa ya Bandari (NBAA), Tumaini University (TUDARCO), Mwl Nyerere Univesity na vingine,” alisema Mambosasa.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: