Ikiwa zimepita siku kadhaa tangu Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Juliana Shonza kutangaza adhabu ya kumfungia kutoshiriki kazi za sanaa kwa kipindi cha miezi sita msanii Roma Mkatoliki pamoja na kufungia baadhi ya nyimbo za wasanii wengine, Leo March 26, 2018 Mwenyekiti wa UVCCM Taifa Kheri James akiwa katika mkutano na wanachama mkoani Dodoma alionesha hisia zake za kutopendezwa na maamuzi hayo.

“Viongozi wanaoshughulika na masuala ya sanaa na utamaduni wasiifanye kazi hii kama kazi ya uhakimu bali waifanye kama kazi ya Ualimu kwa kuwafundisha watu namna ya kufanya”- amesema James na kuongeza;

“Serikali ya CCM imeahidi ajira kwa vijana, Vijana wameamua kujiajiri kwenye sanaa. Walimu wetu ni kuwawezesha kwenye sanaa na sio kuwakatisha tamaa kwahiyo tusitumie kigezo cha sheria na taratibu kuwaangamiza watu ambao tungeweza kuwaelimisha na wakafanya vizuri zaidi.
 
“Leo tuna wasanii ambao wameitangaza nchi yetu vizuri na wanalipa kodi kwa kazi zao sasa leo tunakwenye kupoteza mabalozi wazuri na walipakodi kwa makosa madogo ambayo yanaweza kurekebishwa na tukaendelea kufanya vizuri. Kama tutaaendelea kuwaacha vijana wakiangamizwa kwa kitu kinaitwa kanuni na taratibu za sheria basi hakuna kijana atakayebaki hapa”
Share To:

msumbanews

Post A Comment: