Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akipakwa majivu wakati wa ibada ya Jumatano ya Majivu katika kanisa la Mtakatifu Joseph jijini Dar es salaam asubuhi ya leo.

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli ameungana na waumini wa Kanisa Katoliki na wakristo wengine katika ibada ya Jumatano ya majivu inaoashiria kuanza kwa mfungo mtukufu wa kwaresma.

Rais John Magufuli akisalimiana na Muadhama Askofu Mkuu Polycarp Kardinali Pengo wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam baada ya kujiunga na waumini wengine katika ibada ya Jumatano ya Majivu katika kanisa la Mtakatifu Joseph jijini Dar es salaam asubuhi ya leo Feb 14.

Magufuli akiwa na mkewe, Mama Janeth Magufuli wameungana na waumini hao katika ibada iliyoongozwa na Muadhama Askofu Mkuu, Polycarp Kardinali Pengo wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam katika Kanisa la Mtakatifu Joseph, Dar, leo Februari 14, 2018.
Mama Janeth Magufuli akisalimiana na Muadhama Askofu Mkuu Polycarp Kardinali Pengo wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam baada ya kujiunga na waumini wengine katika ibada ya Jumatano ya Majivu katika kanisa la Mtakatifu Joseph jijini Dar es salaam asubuhi ya leo Feb 14.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: