Klabu ya Simba yenye makazi yake eneo la Msimbazi jijini Dar es Salaam leo Januari 18 imemtambulisha kocha mpya raia wa Ufaransa, Pierre Lechantre.

Kocha huyo amekuja kuchukua mikoba iliyoachwa na raia wa Cameroon Joseph Omog ambaye kibarua chake kiliota nyasi mwishoni mwa mwaka jana, kufuatia timu hiyo kutokufanya vizuri.
Tangu kuondoka kwa Omog, kikosi cha Simba kimekuwa chini ya kocha msaidizi, Massoud Djuma.
Kocha huyo mpya wa Simba anatarajiwa kuanza kazi mara moja na Masoud Djuma ambaye alikuwa akikaimu nafasi hiyo ataendelea kuwa kocha msaidizi.
Pierre Lechantre amezaliwa Aprili 2, 1950 nchini Ufaransa ambapo kabla ya kujikita katika kazi ya ukufunzi, amewahi kuwa mchezaji mpira wa miguu ambapo alikuwa mshambuliaji.
Miongoni wa vilabu ambayo amewahi kuvichezea ni pamoja na Olympique de Marseille, RC Lens, AS Monaco, pamoja na Paris FC vyote vya nchini Ufaransa.
Kocha Lichantre amewahi kufundisha timu/vilabu kadhaa duniani kikiwemo kikosi cha timu ya Taifa ya Cameroon kilichotwaa ubingwa wa Afrika 2000, Congo, Paris FC, Qatar. Pia amefundisha Al-Ittihad Club (Libya), Club Africain, (Tunisia) na Al-Ahli (Saudi Arabia).
Kocha huyo pia alipata kuwa kocha bora wa Afrika mwaka 2001 na pia barani Asia mwaka 2012.
27 Aprili 2012, Lichantre alitangazwa kuwa kocha mkuu wa timu ya taifa ya Senegal lakini hakufanya kazi hiyo baada ya kushindwa kufikia makubalino na Shirikisho la Soka la Senegal.
Lechantre amekuja na kocha wa viungo ambaye ni raia wa Morocco, Mohammed Aymen Hbibi.  Lechantre ameshuhudia mchezo wa Simba leo jioni katika dimba la Uhuru ambapo Simba imeibuka na ushindi mnono wa magoli 4-0 dhidi ya wakulima wa alizeti, Singida United.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: