Baada ya beki wa Kagera Sugar, Juma Nyoso kudaiwa kumpiga shabiki wa Simba hapo jana, Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), limesema linasubiri ripoti ya kamishna wa mchezo huo ili kumchukulia hatua za kinidhamu.
Nyoso alishikiliwa jana na polisi kwa kosa la kumpiga shabiki huyo wa Simba aliwahi kufungiwa kwa miaka miwili kwa makosa ya utovu wa nidhamu.

Afisa Habari wa TFF, Clifford Ndimbo alisema ripoti wa kamishna iteleza kama beki huyo alifanya kitendo hicho cha utovu wa nidhamu.

"Kanuni zipo wazi hivyo hiyo ripoti itafikishwa kwa kamati ya saa 72 ambayo na wenyewe watafanya kazi yao na baadaya hapo tamati itakuwa kwa kamati ya nidhamu," alisema Ndimbo.

Share To:

msumbanews

Post A Comment: