Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Alexander Pastory Mnyeti akizungumza na wananchi wa Wilaya ya Simanjiro kwenye ziara yake ya siku saba ya kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo, kusikiliza kero zao na kuzungumza nao kwa kutoa maagizo na maelekezo mbalimbali kwa wananchi na viongozi wa eneo hilo.
 Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Alexander Pastory Mnyeti akizindua ujenzi wa nyumba ya walimu wa shule ya kidato cha sita ya sekondari Emboreet, Wilaya ya Simanjiro iliyojengwa kwa ufadhili wa shirika lisilo la kiserikali la ECLAT Foundation kwa kuchimba msingi kwa kutumia jembe.
Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Alexander Pastory Mnyeti (mwenye shati la maua) akimsikiliza Mwenyekiti wa shirika lisilo la kiserikali la ECLAT Foundation, Peter Kiroiya Toima, juu ya ujenzi wa chuo cha ufundi cha Veta, ambacho kimejengwa na shirika hilo.


Mkuu wa Mkoa wa Manyara Alexander Mnyeti, amemtumia salamu mbunge wa Jimbo la Simanjiro James Ole Millya (Chadema) kutumia nafasi hii kuagana na wananchi wake kwani hawezi kushinda tena ubunge wake mwaka 2020.

Mnyeti aliyasema hayo wakati akizungumza kwenye uzinduzi wa nyumba sita za walimu wa shule ya sekondari Emboreet kwa ufadhili wa shirika lisilo la kiserikali la ECLAT Foundation.Alisema Ole Millya anapaswa kuanza kupita kwenye vijiji vya jimbo hilo kwa ajili ya kuaga wananchi wake sababu hivi sasa wanataka kuongozwa na mbunge wa CCM.

"Mfikishieni salamu zangu rafiki yangu Ole Millya kwani tulikuwa naye CCM na namuhakikishia hawezi kuwa mbunge wa jimbo la Simanjiro mwaka 2020 kwa sababu CCM italirudisha hivyo aanze kuaga kabla hajaondoka," alisema Mnyeti.Hata hivyo, Ole Millya alisema Mnyeti ni kijana mwenzake wanayeheshimiana na waliyefahamiana kwa muda mrefu tangu wakiwa UVCCM, hivyo haamini kama maneno hayo yametoka kinywani mwake.

Alisema Simanjiro aliyoikuta wakati anachaguliwa mwaka 2015, ilikuwa imeharibiwa kwa siasa za maji taka, rushwa zinazodhalilisha utu wa watu na uuzaji wa ardhi uliokithiri."Kama nia yetu ni maendeleo kwa wananchi tunaowaongoza ni muhimu kushirikiana ili lengo litimie na Mungu akitufikisha mwaka 2020 wananchi waamue nani wa kumpa kura kwenye nafasi ya Udiwani, Ubunge na Urais," alisema Ole Millya.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: