Hatimaye Alexis Sanchez ameonekana akiwa katika uzi wa Manchester United namba 7.

Sanchez anatarajia kutangazwa rasmi ndani ya saa 24 rasmi akiwa mchezaji wa Manchester United.

Katika picha ya uficho, Sanchez anaonekana akipiga picha hiyo akiwa Old Trafford.

Taarifa zinaeleza amepelekwa Old Trafford kwa ajili ya kupiga picha maalum.

Raia huyo wa Chile kutoka Arsenal, anatarajia kuwa akilipwa pauni 600,000 kwa wiki zitakazomfanya kuwa mchezaji anayelipwa zaidi ndani ya klabu hiyo.

Mgawanyo wa fedha hizo uko mshahara pauni 350,000, haki za picha pauni 100,000 na bonas itakuwa pauni 144,000.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: