Mwenyekiti wa Chama cha ACT Wazalendo Ndugu Yeremia Kulwa Maganja atakuwa na ziara ya siku tano kwenye mikoa ya Njombe, Iringa, Ruvuma, Dodoma na Singida kuanzia tarehe 21 hadi 24 Januari 2017.

Katika ziara hiyo iliyobeba jina la "Ziara ya Demokrasia" mwenyekiti atapokea ripoti ya mwenendo wa uhuru wa kisiasa, haki za kiraia na demokrasia kwenye maeneo atayoyatembelea na kuwajenga kimbinu na kimkakati viongozi wa Chama wa maeneo husika.

Mbali na mikakati ya kutetea na kuilonda misingi ya kidemokrasia, Mwenyekiti atapata pia fursa ya kukagua uhai wa chama, kukagua maendeleo ya Mchakato wa uchaguzi wa ndani katika ngazi ya matawi na kusikiliza kero za wanachama na kuzitolea majawabu.

Ratiba ya ziara itakuwa Kama ifuatavyo:

1. Songea tarehe 20
2. Njombe tarehe 21
3. Iringa tarehe 22
4. Dodoma tarehe 23
5. Singida tarehe 24

Ado Shaibu, Katibu wa Itikadi, Mawasiliano na Uenezi
Imetolewa leo tarehe 18 Januari 2018
Share To:

msumbanews

Post A Comment: