Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Finland Pekka Hekka juu ya utekelezaji wa mradi wa TANZIS.

Mazungumzo hayo yamefanyika mkoani Dodoma katika ofisi za Waziri.

Lengo la mradi wa TANZIS ni  kukuza  ujuzi na ubunifu kwa lengo la  kuongeza  mianya ya ajira, na kuwa mradi huo unatarajiwa kuanza mapema mwaka huu  na utafadhiliwa na Serikali ya Finland.

Kikao hicho pia kilihudhuriwa na  Dkt Amos Nungu ambaye ni  Mkurugenzi  Msaidizi  idara ya  Sayansi,  Teknolojia na Ubunifu.

 Imeandaliwa na;

Kitengo cha Mawasiliano Serikalini.

WIZARA YA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA.

16/1/2018
Share To:

msumbanews

Post A Comment: