Basi kampuni ya Tahmeed  lililokuwa likitoka jijini Dar es Salaam kwenda Mombasa, Kenya limeteketea kwa moto leo Januari 29, mwaka 2018  katika kijiji cha Kitumbi wilayani Handeni mkoani Tanga.

Mkuu wa Jeshi la Polisi wilayani Handeni, William Nyero amesema polisi wapo eneo la tukio na hakuna madhara yoyote kwa abiria waliokuwa kwenye basi hilo.

Amesema dereva wa basi hilo baada ya kubaini kasoro aliliegesha pembeni na abiria kuteremka, kushusha mizigo yao.

"Abiria wote waliokuwa wakisafiri na basi hilo wapo salama. Baada ya abiria kushuka na kushusha mizigo yao basi liliwaka moto,” amesema.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: