Na Emmanuel J Shilatu
 Iringa, Tanzania

Vijana wametakiwa kuchangamkia fursa za Mafunzo ya Ufundi, pamoja na mafunzo ya UWELEDI mahali katika sehemu zao za kazi ili kuweza kukabiliana na changamoto ya ukosefu wa Ajira kwa Vijana.

Akizungumza na vijana wa chuo cha Ufundi cha Don Bosco Mkoani Iringa, ambao wanapatiwa Mafunzo Chini ya Ufadhili wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mtaalamu Mshauri wa Mawasiliano kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Kazi, Ajira na vijana Ndugu Jerry C. Muro amesema Serikali inalenga kuwafikia Vijana Milioni tano katika kipindi hiki kabla ya mwaka 2020 hatua itakayosaidia kuongeza Nguvu kazi ya vijana Weledi na wajuzi katika soko la ndani la Ajira pamoja na kutoa fursa kwa vijana kuweza kujiajiri hatua itakayosaidia kupunguza Makali ya changamoto ya Ajira nchini.



Share To:

msumbanews

Post A Comment: