Waandamanaji wakidai mwisho wa ukandamizaji dhidi ya watu kutoka jamii ya Oromo, mjini Addis Ababa, Agosti 6, 2016.
Makabiliano
 kati ya polisi na waandamanaji yamesababisha watu wengi kufariki dunia 
nchini Ethiopia, wakati wa tamasha la jadi la Oromo Ireecha. Tukio hilo 
limetokea Jumapili asubuhi katika mji wa Bishoftu, kusini mwa mji wa 
Addis Ababa, lakini taarifa ya watu waliopoteza maisha bado 
haijathibitishwa na serikali.
Ni vigumu
 kusema kwa sasa ni watu wangapi wamepoteza maisha Jumapili hii asubuhi 
katika mji wa Bishoftu mkoani Oromo, jina la kabila la kwanza kwa watu 
wengi nchini Ethiopia. Makabiliano yalilipuka wakati wa sikukuu ya 
kidini inayoashiria mwisho wa msimu wa mvua.
Umati wa 
watu waliokuepo katika sherehe hizo walipinga uwepo wa viongozi kutoka 
jamii ya Oromo wanaoshirikiana na serikali, ambao wanawachukulia kama 
wasaliti. Waandamanaji walijaribu kuvamia jukwaa waliokuemo viongozi 
hao, lakini polisi walijibu kwa mabomu ya machozi.
Ilifuatiwa
 hali ya wasiwasi na hofu na kusababisha watu kukanyagana ambapo wakati 
huo watu kadhaa walipoteza maisha. Mpiga picha wa shirika la habari la 
AFP anasema aliona miili angalau ishirini ya watu waliofariki.
Upinzani 
nchini Ethiopia kwa upande wake, unadai kuwa watu zaidi ya 100 
walifariki katika mkanyagano huo. Tamasha lilivunjwa na tukio hili 
linakumbusha hali ya mivutano inayoshuhudiwa katika mkoa wa Oromo wakati
 ambapo maandamano dhidi ya serikali ambayo yalianza karibu mwaka mmoja 
uliyopita yameendelea kushika kasi.
Kwenye 
mitandao ya kijamii, wanaharakati kutoka jamii ya Oromo wametoa wito wa 
hasira wa siku tano, huku idadi kubwa ya polisi ikionekana Jumapili hii 
mchana katika mkoa wa Oromo na karibu ya mji mkuu wa Ethiopia, Addis 
Ababa
Posted By Lyidia Kishia 
 
 
 
 
  
 
 
 
 
 
 
 
 Back To Top
 
Post A Comment: