Watoto 22 na Mwalimu wao wa Madrasa Watiwa Mbaroni Kwa Madai ya Kujifunza UGAIDI.
JESHI
la polisi mkoani Pwani ,limewakamata watoto 22 wa madrasa ya Arahma
pamoja na mwalimu wa madrasa hiyo Ashura Said(47) ambae alikuwa
akiendesha mafunzo ya kigaidi kwa watoto hao,huko Kimarang’ombe ,kata ya
Nianjema ,Bagamoyo.
Aidha jeshi hilo limefanikiwa kukuta bomu moja la moshi lenye namba G2020c.SS-STCS katika makazi anayoishi mwalimu huyo .
Akizungumzia
tukio hilo,kamanda wa polisi mkoani Pwani,Boniventure Mushongi,alisema
Ashura anashikiliwa na polisi kwa mahojiano zaidi kuhusiana na kuhusika
kuendesha mafunzo ya kigaidi kinyume na sheria.
Alieleza
kuwa taarifa hiyo ilitolewa na raia wema juu ya mwenendo wa mwalimu
huyo wa madrasa na baada ya kumfanyia upekuzi polisi walifanikiwa kukuta
na bomu moja la moshi.
Kamanda
Mushongi,alisema uchunguzi wa awali ulibaini makazi hayo yanamilikiwa
na taasisi ya kiislamu iitwayo Akha Laagul Islam,iliyosajiliwa kwa lengo
la utoaji huduma kwa watoto yatima kutoka maeneo mbalimbali ikiwemo Dar
es saalam ,Tanga,Handeni,Mlandizi na Bagamoyo kwa mkoa wa Pwani.
“Badala yake watoto hao wamekuwa wakitumika kwa mafunzo yasiyofaa kwa watoto wa kituo hicho”alisema kamanda Mushongi.
Hata
hivyo alisema jeshi la polisi limewamakata watoto 22 ambao walikuwa
wakijaribu kukimbia ambao kati yao 16 ni wakike na 6 ni wa kiume kwa
ajili ya uchunguzi wa tukio.
Katika
tukio jingine ,Bakari Saidi (45)mkazi wa Kimanzichana Kusini ,wilayani
Mkuranga, ameuwawa kwa kupigwa risasi kifuani upande wa kulia na kutokea
chini ya bega la kushoto ,mgongoni na watu wasiofahamika.
Katika
tukio hilo,Omar Ally (55)ambae ni afisa mtendaji wa kijiji cha
Kimanzichana Kusini,alijeruhiwa kwa kupigwa risasi kwenye mkono wake wa
kushoto na amelazwa katika hospitali ya wilaya hiyo kwa matibabu.
Kadhalika katika eneo la tukio kumekutwa maganda mawili ya risasi yanayotumika kwenye silaha ya SAR/SMG .
Kamanda
Mushongi alisema watu hao walivamia katika ofisi ya serikali ya kijiji
cha Kimanzichana Kusini na kufanya mauaji hayo ambapo mtu huyo
alifariki dunia na mwingine mmoja kujeruhiwa.
Anasema tukio hilo limetokea octaba 5 mwaka huu katika kitongoji cha Ukwama kata ya Kimanzichana tarafa ya Mkamba wilayani hapo.
“Wakati
marehemu akiwa anajaza fomu za mkopo wa benki ya akiba Commerce
bank(ACB),ghafla walitokea watu wawili wakiwa na silaha mbili na kuanza
kuwafyatulia risasi na kutoweka kusikojulika wakitumia usafiri wa
pikipiki"alisema kamanda Mushongi.
Kamanda
huyo alifafanua kuwa mwili wake umehifadhiwa katika hospitali ya wilaya
ya Mkuranga na utakabidhiwa kwa ndugu zake kwa ajili ya mazishi mara
baada ya uchunguzi kukamilika.
Jeshi
hilo limewahakikishia wananachi wote usalama wao na kwamba linapambana
kwa nguvu na wale wenye nia ya kuwatia hofu wananchi,kwani hawataweza
kufanikiwa katika mipango yao .
Limewaasa
wananchi kuwafichua wahalifu ambao ni sehemu ya jamii wanapoishi badala
ya kuoneana muhali pamoja na kutoa taarifa pale wanapobaini kuna watu
ama raia asiyemwema
Post A Comment: