Home
Kitaifa
Jambazi Kigoma Awajeruhi Kwa Bomu Askari na Raia Wanne 
 
Polisi na raia wanne wamejeruhiwa kwa 
bomu la kutupwa kwa mkono walipokuwa wakimkamata mtuhumiwa wa ujambazi 
kwenye Kijiji cha Uvinza mkoani Kigoma. Kamanda wa Polisi Mkoa wa 
Kigoma, Ferdinand Mtui alisema jana kuwa tukio hilo lilitokea Oktoba 14. 
Alimtaja mtuhumiwa huyo kuwa ni Yahya Kamuhanda (49) mkazi wa kijiji 
hicho. Mtui aliwataja majeruhi hao kuwa ni askari polisi F.3187 Koplo 
Isaya na raia Saidi Mohamed, Seleman Kashali, Joseph Daudi na Hassan 
Nasibu, wote wakazi wa Kijiji cha Uvinza. 
Alisema askari walipata 
taarifa kutoka kwa raia wema kwamba Kamuhanda anajiandaa kufanya uhalifu hivyo waliweka mtego eneo la Uvinza 
Madukani alikokwenda kununua mahitaji. 
Alidai kuwa alipotambua anafuatiliwa alitupa bomu ndipo polisi walimpiga risasi mguuni na wananchi 
walimvamia na kumshambulia kabla ya askari kutumia nguvu kumwokoa 
asiuawe kwa kipigo. 
Mtui alisema mtuhumiwa alipohojiwa alisema 
alificha bunduki kijijini kwao Lukole wilayani Ngara mkoani Kagera, 
ambako askari walikamata SMG yenye namba 78GA5062 ikiwa imefukiwa 
ardhini.
 Pia, walikamata magazini saba, moja ilikuwa na risasi 40, nne 
(risasi 30 kila moja) na mbili (risasi 20 kila moja) na risasi 75 
zilikuwa kwenye mfuko wa sandarusi. Pingu moja na funguo zake, maski 
tisa na laini 20 za mtandao wa Halotel ambazo hazijasajiliwa. 
Mtui 
alisema mtuhumiwa huyo alifariki dunia juzi akipatiwa matibabu kwenye 
Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kigoma (Maweni). Alisema majeruhi wote 
watano walipata matibabu hospitalini hapo na waliruhusiwa kurudi 
nyumbani. 
Source P.T 
 
 
 
 
 
  
 
 
 
 
 
 
 
 
 Back To Top
 
Post A Comment: