Watu
 10 wamefariki dunia na wengine 44 wamejeruhiwa baada ya basi la kampuni
 ya Barcelona walilokuwa wakisafiria kutoka jijini Dar es Salaam kwenda 
mkoani Lindi  kupata ajali eneo na Miteja mkoani Lindi.
 
Taarifa
 iliyotolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Lindi, Renata Mzinga imesema 
kuwa chanzo cha ajali hiyo kimetokana na tairi ya gari ya upande wa 
kushoto kupasuka na kutokana na mwendo wa kasi wa basi hilo, dereva 
alipoteza uelekeo ndipo likapinduka.
Pia
 Kamanda Mzinga amesema kuwa wamechunguza na kugundua kua licha ya kuwa 
basi hilo lilikuwa na uwezo wa kubeba abiria 48, wakati basi hilo 
linapata ajali kulikuwa na abiria 54 kitu ambacho ni kosa kisheria.
Aidha,
 Kamanda Mzinga amesema kuwa bado wanaendelea na uchunguzi kuweza 
kubaini alipo dereva ili kuweza kufahamu ni kipi hasa kilichotokea. Hadi
 sasa wanamshikilia kondakta wa basi hilo lakini bado hajaweza kuelezea 
tukio halisi.
 
 
Post A Comment: