Rais
 wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli kesho 
anatarajiwa kuzindua ndege mbili mpya aina ya Bombardier Q 400 
zilizonunuliwa na Serikali hivi karibuni.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Uchukuzi) Dkt. Leornard Chamuriho amesema maandalizi yote kwa ajili ya uzinduzi wa ndege hizo yamekamilika na uzinduzi huo utafanyika katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Kesho kuanzia saa mbili asubuhi.
“Tunawaomba wanahabari na wananchi kujitokeza kwa wingi katika uzinduzi huo ili waone utekelezaji wa ahadi wa Serikali katika mkakati wa kuhuisha usafiri wa Anga hapa nchini”, amesema Dkt. Chamuriho.
Ndege hizo aina ya Bombardier Q 400 zenye uwezo wa kubeba abiria 76 kila moja zimetengenezwa nchini Canada na zitahudumia soko la ndani ndani na nchi za jirani zitakapoanza kazi.Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.

Katibu
 Mkuu Uchukuzi, Dkt. Leonard Chamriho akiwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa 
ATCL Mhandisi Ladislaus Matindi pamoja na maafisa wengine wakiwa katika 
Ndege ya pili ya Bombadier Q400 iliyonunuliwa na serikali kwa ajili ya 
Shirika la Ndege la Taifa (ATCL) mara ilipotua katika uwanja wa ndege wa
 kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Septemba 27, 2017 
ikitokea Canada ilikotengenezwa.
Katibu
 Mkuu Uchukuzi, Dkt. Leonard Chamriho na viongozi wengine wakielekea 
kwenye Ndege ya pili ya Bombadier Q400 iliyonunuliwa na serikali kwa 
ajili ya Shirika la Ndege la Taifa (ATCL) ilipowasili katika uwanja wa 
ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Septemba 
27, 2017 ikitokea Canada ilikotengenezwa. Sherehe za uzinduzi rasmi wa 
ndege hizo umepangwa kuganyika kesho Jumatano Septemba 
www.msubanews.blogspot.com

Post A Comment: