Mshtakiwa Miriam Mrita akitoka katika ukumbi wa wazi wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam baada ya kesi ya mauaji inayomkabili ya kumuua aliyekuwa mdogo wa mume wake Bilionea Msuya, Aneth Msuya yaliyotokea 2016 huko Kibada Kigamboni.


 MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam imeelezwa kuwa, mshtakiwa Miriam Mrita ambaye ni mke wa marehemu bilionea Msuya wakati anahojiwa na polisi aliwapeleka Kibada- Kigamboni ambako ndiko eneo tukio lilipotokea.


Imeelezwa akiwa Kigamboni alihojiwa kwa takribani dakika 10 hadi 15 huku akirekodiwa kwenye video.

Shahidi wa sita wa upande wa Jamuhuri, Inspekta Alistides Kasigwa ambaye ni mchunguzi wa picha mbalimbali zinazohusu matukio ya kihalifu na zile zisizokuwa na kihalifu ameeleza hayo leo Machi 8, 2022 wakati akitoa ushahidi wake katika kesi ya mauaji inayomkabili aliyekuwa mke wa bilionea Msuya, Miriam Mrita na mfanyabiashara Revocatus Muyella mbele ya Jaji Edwin Kakolaki.

kwenye kesi hiyo Mrita na Muyella wanadaiwa kumuua kwa kumchinja dada wa marehemu bilionea Msuya, Aneth Msuya nyumbani kwake Kigamboni jijini Dar es Salaam tahere 25 Mei 2016 ikidaiwa Allan Kimario (4) akishuhudia

Akiongozwa na wakili wa serikali Mwandamizi Genes Tesha, Kasigwa amedai yeye anafanya kazi katika jeshi la polisi kamisheni ya uchunguzi wa kisayansi kwa zaidi ya miaka 15.

Amedai kuwa, Agosti 8, 2016 akiwa ofisini, alipewa barua na SSP Bukombe kutoka kwa Mkurugenzi wa upelelezi wa makosa ya jinai, ikimtaka kwenda kurekodi video ya mahojiano hayo ya mshtakiwa Mrita na SP Latifa.

Amesema alichukua vifaa vyote vya habari na kwamba alitumia video kamera yake aliyoitaja aina ya Sony , betri, tape za min-div , chaja ya kamera na stendi yake kwa ajili ya kazi hiyo.

Amedai aliamuriwa kwenda kituo cha Polisi cha uwanja wa ndege jijini Dar es Salaam, ambapo aliwakuta askari David Mhang’aya Jumanne Malaghahe na baadaye aliingia kwenye chumba cha mahojiano alimkuta mtuhumiwa wa Mrita pamoja na SP Latifa ndipo wakaanza mahojiano hayo huku yeye akirekodi kupitia kamera yake na kwamba alidai kuwa alitumia dakika 40 kurekodi mahojiano hayo.

Alipoulizwa kama akimuona mshtakiwa angemtumia alisema ndio na kwenda kumtambua mshtakiwa mahakamani hapo kwa kumsogelea na kumnyooshea mkono.

Pamoja na maelezo mengine, Shahidi Kasigwa alidai baada ya kumaliza mahojiano hayo alirejea Ofisini kwake na kuandaa nakala mbili kwenye DVD, na tape moja akadai kuwa alizifunga vizuri kwa seald na kuweka saini yake juu ya bahasha.


Inspekta Kasigwa aliiomba mahakama kupokea bahasha hiyo kama kielelezo ambapo Jaji Kakolaki alipokea

Baadaye Wakili Tesha aliomba mahakama hiyo imrejeshee tena bahasha hiyo ambapo alirejeshewa na kumtaka Shahidi huyo aifungue na aeleze kilichopo ndani ya bahasha hiyo,Shahidi huyo alifungua bahasha hiyo na kutoa tape ambayo alidai kuwa ndiyo aliyoitumia kurekodi mahojiano ya Mtuhumiwa na SP Latifa.
Wakili Tesha akamuhoji kwamba anataka mahakama iifanye nini Tape hiyo akajibu kuwa ipokelewe kama kilelezo.

Wakili Kibatala alipinga kupokelewa kwa kielelezo hicho na akidai kuwa utaratibu uliotumika umekinzana na sheria ya ushahidi ambapo amedai kuwa ushahidi wa tape ni ushahidi wa kieletroniki ambao haujajitosheleza kwenye uwasilishwaji wake "Tulitegemea wakati shahidi anaongozwa angetueleza kuwa wakati anakwenda kurekodi kamera yake aliichaji au ilikuwa na chaji na hakueleza kama wakati anarekodi kamera hiyo ilikuwa ikifanya kazi vizuri au la.

Katika hoja nyengine Kibatala amedai sheria ya ushahidi wa kieletroni kwenye kurekodi mpiga picha anatakiwa asiwe kwenye upande wenye maslahi na kesi hiyo ambapo ameeleza shahidi huyu yupo chini ya DPP

Na kwamba Jamuhuri walipaswa kuainisha kielelezo hicho cha kielektroniki kilipaswa kuwasilishwa kwa kiapo juu ya ushahidi huo na kwamba upande wa Jamhuri ulipaswa kueleza kwenye maelezo ya mwenendo wa mashtaka (Committal).

Hata hivyo wakili Tesha akijibu hoja hizo amedai Mapingamizi hayo hayana mashiko kwani shahidi ametoa ushahidi wake kwa mujibu wa sheria na hakufanya kazi chini ya DPP, alitekeleza majukumu yake chini ya Mkurugenzi wa upelelezi wa makosa ya jinai.

Kufuatia mabishano makali ya kisheria, Kakolaki ameahirisha kesi hiyo hadi kesho saa tatu asubuhi kwa ajili ya uamuzi.


Share To:

Post A Comment: