Wajumbe wa Kamati ya Siasa Kata ya Mandewa mkoani Singida wakishiriki ujenzi wa Kituo cha Afya cha eneo la Mwaja walipofanya ziara ya kukagua ujenzi wa kituo hicho leo.
Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kata ya Mandewa Yusuph Kijanga Makera (katikati) akisaidia kumsogezea matofali fundi wakati wa ziara hiyo.
Mwenyekiti wa CCM Kata ya Mandewa Hamisi Ireme akizungumza kwenye ziara hiyo. Kulia ni Balozi wa Shina namba moja Mtaa wa Unyankhaye  Juma Mataka na kushoto ni Diwani wa kata hiyo, Baraka Hamisi.
Diwani wa Kata ya Mandewa Baraka Hamisi akizungumza kwenye ziara hiyo 
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Unyankhaye Aboubakar Athumani akichangia jambo kwenye ziara wakati wa ukaguzi wa Soko la wafanyabiara ndogondogo la Samaki Samaki.
Wafanyabiashara ndogondogo wa soko hilo wakiwasikiliza viongozi waliokuwa kwenye ziara hiyo baada ya kusikiliza kero zilizopo katika soko hilo.
Ukaguzi wa ujenzi wa Kituo cha Afya Mwaja ukiendelea.
Ujenzi wa Kituo cha Afya Mwaja ukiendelea.
Katibu wa CCM Kata ya Mandewa, Yusuph Kijanga Makera akizungumza kwenye ziara hiyo.
Ukaguzi wa eneo la Kituo cha Afya  Mwaja ukiendelea.
Mjasiriamali Ester Ramadhani wa Soko la Samaki Samaki akizungumzia changamoto ya ukosefu wa miundombinu ya soko hilo.
Katibu wa Hamasa CCM Kata ya Mandewa Jamaldin Nyanga akizungumza na mmoja wa wajasiriamali wa Soko la Samaki Samaki Kuluthum Juma wakati wa ziara hiyo.
Mjasiriamani Kuluthum Juma akiwa kwenye kibanda chake cha biashara kwenye soko hilo.
Mafundi wakiendelea na ujenzi wa kituo hicho cha afya.
Mjumbe wa kamati ya siasa, Hamisi Msaghaa ' Maarufu  Muna Dalali' akishiriki ujenzi wa kituo hicho cha afya.
Mmoja wa wasimamizi wa ujenzi wa kituo hicho cha afya, Hamadi Hamisi, akizungumzia maendeleo ya ujenzi wa kituo hicho.
Mwenyekiti wa CCM Tawi la Mwaja Juma Asi (katikati) akizungumza kwenye ziara hiyo. Kulia ni Mwenyekiti wa CCM Kata ya Mandewa, Hamisi Ireme na kushoto ni Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Mwaja, John Pascal.
Wajumbe wa Kamati ya Siasa Kata ya Mandewa pamoja na wananchi wakiwa katika picha ya pamoja baada ya ziara hiyo.
 

Na Dotto Mwaibale, Singida


CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) Kata ya Mandewa mkoani Singida kupitia kamati ya siasa ya kata hiyo wamempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutoa Sh. 600 Milioni kwa ajili ya kujenga Kituo cha Afya eneo la Mtaa wa Mwaja katika kata hiyo.

Kukamilika kwa ujenzi wa kituo hicho cha afya wananchi wa eneo hilo hasa wajawazito wataondokana na adha ya kutembea umbali mrefu wa kwenda kupata huduma za afya Hospitali ya Sokoine iliyopo mjini hapa.

Akizungumza wakati wa ziara iliyofanywa na kamati hiyo ya kukagua ujenzi wa kituo hicho cha afya    juzi Mwenyekiti wa CCM wa kata hiyo Hamisi Ireme alimshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwakumbuka wananchi wa eneo hilo na kuwapa kiasi hicho cha fedha za ujenzi. 

Akizungumzia soko hilo jipya la Samaki Samaki lililopo Unyankhaye ambalo linatumiwa na wafanya biasha ndogo ndogo walioondolewa kwenye maeneo yasio rasmi kwa agizo la Serikali Ireme alitumia nafasi hiyo kuwahasa maafisa wa Serikali kushirikiana na viongozi wa Serikali za mitaa na madiwani kwenye kata zao ili kuondoa migongano isiyo ya lazima wakati wa kutekeleza shughuli mbalimbali za kimaendeleo.

"Kwa nafasi ya kipekee nimshukuru Mbunge wa Jimbo la Singida Mjini Mussa Sima kwa kutoa fedha za mfuko wa jimbo ambazo zinasaidia kuchonga barabara katika viwanja vilivyopimwa jambo litakalosaidia kuleta maendeleo kwenye kata yetu" alisema Ireme.

Diwani wa Kata ya Mandewa Baraka Hamisi akizungumzia ziara hiyo alisema imeleta hamasa na kama Serikali wamekuwa na mambo wanayoyafanya hasa pale zinapoibuka changamoto mbalimbali huwa wanatafuta sehemu ya kuzipeleka ambapo ni kwenye chama. 

Alisema katika Soko la Samaki Samaki wamebaini changamoto za watu kutoka nje ya kata hiyo kupewa maeneo ya kujenga vibanda na kuondoka na hali hiyo ilitokana na viongozi wa eneo hilo kutoshirikishwa jambo ambalo limechangia kwa wafanyabiashara waliowengi kutotumia eneo hilo na kurudi kwenye maeneo yao ya awali.

"Suala la wafanyabiashara hao kutengewa maeneo rasmi ni agizo la Rais lakini tumeshindwa kuwarudisha kwa kuwa mchakato mzima wa kuwahamishia katika soko hilo hatukushirikishwa lakini kwa kuwa lipo ndani ya uwezo wetu tutalifanyia kazi" alisema Hamisi.

Katibu wa CCM wa kata hiyo Yusuph  Kijanga Makera aliushukuru uongozi wa CCM kuanzia ngazi ya wilaya, mkoa na ngazi ya Taifa chini ya Rais Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa walioifanya ya kuwapatia mradi mkubwa ambapo wanapokea pongezi nyingi kutoka kwa wananchi hasa Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan anavyoitekeleza ilani ya CCM.

Alisema katika Soko la Samaki Samaki wameona changamoto nyingi za kutokuwepo kwa vyoo, maji,umeme, guba la takataka na baadhi  ya watu kutoka nje ya eneo hilo kupewa vibanda ambapo wajasiriamali wa eneo hilo wameomba kufanyike uhakiki mpya ili waweze kutambuliwa.

Mjumbe wa Serikali ya Mtaa wa Mwaja Subira Mukhenyi aliishukuru Serikali kwa kuwajengea kituo hicho kwani kukamilika kwake kitatoa msaada mkubwa wa matibabu hasa kwa wajawazito.

Share To:

dottomwaibale

Post A Comment: