Wednesday, 22 December 2021

Madiwani fanyeni Maamuzi yenye Tija

 


MKALAMA


Mivutano yetu haiwasaidii wananchi wanachotaka kuona ni maendeleo tu sasa Kila diwani akitaka Kituo kikajengwe kwenye Kata yake  haiwezekani Vituo hivi vinajengwa kwa kuzingatia vigezo vilivyowekwa.


Mhe. Ummy alisema hayo wakati wa ziara yake Wilayani Mkalama na kukagua maendeleo ya ujenzi wa kituo cha Afya  Ilunda ambacho ujenzi wake umechelewa kutokana na mvutano wa Baraza la Madiwani.


Amesema maslahi ya viongozi yasikwamishe utekelezaji wa shughuli za maendeleo kwa sababu Serikali inaleta fedha kwa ajili ya utekelezaji wa miradi lakini baadhi ya viongozi wanatanguliza maslahi yao mbele badala ya kuzipa kipaumbele changamoto zinazowakabili wananchi hili halileti Afya kwenye Halmashauri zetu’ alisisitiza Mhe. Ummy.


Mhe. Ummy alihitimisha kuwa maslahi binafsi ya viongozi wetu kwa namna yeyote ile yasikwamishwe utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika Mamlaka za Serikali za Mitaa tuzingatie maslahi mapana ya wananchi.

No comments:

Post a Comment