Dkt Juma Mhina Mkurugenzi halmashauri ya ngorongoro akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake  kuhusu  uchaguzi Katika jimbo la ngorongoro.

 Zaidi ya wagombea wa vyama 13 vya Siasa wamejitokeza kugombea ubunge katika jimbo la Ngorongoro katika uchaguzi mdogo unatarajiwa kufanyika Disemba 11 mwaka.


Uchaguzi huo mdogo unafanyika kufuatia aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo Willium Ole Nasha kufarikia nyumbani kwake Jijini Dodoma Septemba mwaka 2021.

Taarifa iliyotolewa na msimamizi wa uchaguzi wa jimbo la Ngorongoro Dk,Juma Mhina aliwataja wagombea hao kuwa ni pamoja na

Emmanuel Shangai (CCM) Simon Bayo (SAU) Singa Kalekwa (CCK), Amina Mcheka (NLD) Mary Daudi (UPDP).

Dk, Mhina aliwataja wagombea wengine kuwa ni Mgina Mustafa (AAFP),.Frida Nnko (UMD),Paulo Makuru (UDP),Shafii Kitundu (ADC), Feruziy Feruziyson (NRA),

Simon P Ngilisho (DEMOKRASIA MAKINI), Jonson Gagu (ACT WAZALENDO) na Zuberi Hamis (ADA TADEA).

"Tangu tumeanza zoezi hili Novemba 9 hadi jana Novemba 11 mwaka huu wagombea 13 kutoka vyama mbalimbali vya siasa wamejitokeza kuchukua fomu za kuwania ubunge wa jimbo hili la Ngorongoro,Ofisi ya NEC jimbo la Ngorongoro inaendelea kukaribisha vyama vingine vya Siasa kujitokeza kuchukua fomu ya kuwania nafasi hiyo ya ubunge".

Dk Mhina alisema NEC itaendelea kutoa fomu hizo hadi Novemba 15 mwaka huu saa 10:00 jioni na siku hiyo hiyo watatafanya uteuzi wa wagombea waliopitishwa na NEC kugombea ubunge wa jimbo la Ngorongoro.

Ameongeza kuwa uchaguzi huo utakaofanyika November 15 mwaka huu wagombea watakopitishwa kushiriki uchaguzi wataanza kampeni Novemba 16 hadi Disemba 10 mwaka na uchaguzi utafanyika Disemba 11 mwaka huu.
Share To:

TANGA RAHA BLOG

Post A Comment: