Monday, 8 November 2021

TANZANIA KUENDELEA KUTEKELEZA DIPLOMASIA YA UCHUMI KUJILETEA MAENDELEO

 

Mkurugenzi wa Diplomasia ya Uchumi katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Edwin Rutageruka akizungumza wakati wa Mdahalo wa Kitaifa kuhusu “Umuhimu wa Diplomasia ya Uchumi na Ushirikiano wa Kimataifa katika kuwaletea Wananchi Maendeleo”. Mdahalo huo ambao umeandaliwa na Taasisi ya Watch Tanzania umefanyika kwa njia ya mtandao hivi karibuni na kuwashirikisha wadau mbalimbali wakiwemo Mabalozi, Wanadiaspora, Wahadhiri na Wabunge.

Balozi Rutageruka akimsikiliza Mbunge wa Mtama, Mhe. Nape Nnauye alipokuwa anachangia hoja wakati wa mdahalo huo

Naibu Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania kwenye Umoja wa Mataifa, Geneva,
Uswisi, Mhe. Hoyce Temu naye akizungumza wakati wa mdahalo wa kitaifa kuhusu Diplomasia ya Uchumi

Balozi wa Tanzania nchini Korea ya Kusini, Mhe. Togolani Mavura akizungumza wakati wa mdahalo huo

Mtanzania anayeishi Marekani Bi. Loveness Mamuya naye akichangia jambo wakati wa mdahalo kuhusu Diplomasia ya Uchumi huku Balozi Rutageruka akimsikiliza.

Mkurugenzi wa Idara ya  Diplomasia ya Uchumi katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa AfrikaMashariki, Balozi Edwin Rutageruka ametoa wito kwa wadau mbalimbali kushirikiana katika kutekeleza Diplomasia ya Uchumi ili kuliletea Taifa maendeleo ya kiuchumi kupitia mahusiano na nchi mbalimbali, mashirika ya kikanda na
kimataifa.

Balozi Rutagaruka ametoa wito huo hivi karibuni wakati wa Mdahalo wa Kitaifa kuhusu “Umuhimu wa Diplomasia ya Uchumi na Ushirikiano wa Kimataifa katika Kuwaletea Wananchi Maendeleo” uliofanyika kwa njia ya mtandao na kuwashirikisha wadau mbalimbali wakiwemo Wabunge, Mabalozi na Wanadiaspora.

Akizungumza kwenye Mdahalo huo akiwa jijini Dodoma, Balozi Rutagerua amesema kuwa, upo umuhimu mkubwa kwa Tanzania kuendelea kuimarisha mahusiano yake na nchi mbalimbali na mashirika ya kikanda na kimataifa ili inufaike kiuchumi kupitia fursa lukuki zilizopo nchini kama vivutio vya Utalii, fursa za Uwekezaji na Biashara pamoja na kuhakikisha wadau wote zikiwemo Taasisi za Umma na Binafsi, Mabalozi na Wananchi kwa ujumla wanashiriki kikamilifu katika kutekeleza mikakati mbalimbali iliyopo ili kufikia
malengo kusudiwa kupitia Diplomasia ya Uchumi.

Ameongeza kusema kuwa, tayari mafanikio mengi yamepatikana kupitia utekelezaji wa Diplomasia ya Uchumi ikiwemo kuimarika kwa Sekta za Uchumi ambapo tayari mikataba kadhaa ya manufaa kwa nchi imesainiwa ukiwemo ule wa Serikali ya Tanzania kuwa Mwenyeji wa Kampuni ya Mafuta Ghafi ya Afrika Mashariki (EACOP) itakayohusika na Ujenzi wa Mradi wa Bomba la kusafirisha Mafuta Ghafi kutoka Hoima, Uganda hadi Chongoleani Tanga. Mafanikio mengine ni kuondolewa kwa vikwazo 46 kati ya 64 vya muda mrefu visivyo vya kiforodha kati ya Tanzania na Kenya. Vikwazo hivi vimeondolewa kufuatia ziara ya Mhe.
Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Kenya mwezi
Mei 2021.

Kadhalika amesema kuwa, Tanzaniaimeimarisha ushiriki wake katika masuala ya kikanda na kimataifa na kwambamwezi Septemba 2021 Tanzania iliridhia Mkataba wa kuanzisha Eneo Huru laBiashara Barani Afrika na kwamba kuridhiwa kwa mkataba huu kumeongeza ushawishiwa Tanzania katika mtangamano wa Afrika na kuwa sehemu ya soko kubwa la Afrika lenye idadi ya watu wapatao bilioni 1.3. Aliainisha maeneo mengine ya mafanikio
kuwa ni pamoja na kukua kwa matumizi ya Lugha ya Kiswahili na ufunguzi wa
Balozi na Konseli Kuu ambapo hadi sasa Tanazania inazo Balozi 44 na Konseli Kuu
6.

Mbali na mafanikio hayo, Balozi Rutageruka amesema Serikali itaendelea
kutekeleza kikamilifu mikakati iliyopo ya kutekeleza Diplomasia ya Uchumi ikiwani pamoja na kuvutia utalii, uwekezaji na biashara kwa kutumia maonesho namakongamano; kutoa elimu kwa umma kuhusu fursa zinazopatikana katika Jumuiya zaKikanda na Kimataifa; kutafuta fursa za masomo na ufadhili; kubadilishana ujuzikatika nyanja mbalimbali kati ya Taasisi za Tanzania na Taasisi nyingine nje yanchi na kutumia Balozi za Tanzania katika kutangaza vivutio vya utalii na fursaza uwekezaji na biashara zilizopo nchini.

Kwa upande wake, Balozi wa Tanzania nchini Korea ya Kusini, Mhe.
Togolani Mavura ambaye wakati wa mdahalo huo alizungumzia umuhimu wa Diplomasiaamesema ni muhimu kwa Tanzania kuendelea kuwekeza kwenye Diplomasia hususankuimarisha ushirikiano na nchi zingine ili kuepusha migogoro ambayo husababishanchi kupoteza mwelekeo na badala ya kuokoa fedha kwa ajili ya huduma muhimu zajamii kama maji, afya na umeme nchi zinajikuta zinawekeza kwenye masuala yamigogoro na vita ambayo hugharimu fedha nyingi.

Naye Naibu Mwakilishi wa Kudumuwa Tanzania kwenye Umoja wa Mataifa, Geneva, Uswisi, Mhe. Hoyce Temu amesema Tanzaniachini ya Utawala wa Rais wa Awamu ya Sita, Mhe. Samia Suluhu Hassan imeendeleakung’aa kimataifa na kwamba mashirika mbalimbali ya kimataifa yameonesha nia yakuisaidia Tanzania kufikia malengo yake hususan kwenye agenda mbalimbali ikiwemoya Malengo ya Maendeleo Endelevu ya Mwaka 2030.

Akichangia hoja wakati wamdahalo huo, Bi. Loveness Mamuya ambaye ni Mtanzania anayeishi Marekani amesemaJumuiya ya Watanzania wanaoishi nje (Diaspora) ipo tayari kushirikiana naSerikali katika kuchangia maendeleo ya nchi na kutoa rai kwa Serikalikuwashirikisha kikamilifu Diapora kwenye mipango mbalimbali ikiwemo kutafutawawekezaji na wafanyabiashara wa uhakika kutoka kwenye maeneo waliyopo.

Mdahalo huo ambao umeandaliwana Taasisi ya Watch Tanzania na kuwashirikishawazungumzaji mbalimbali umeongozwa na Dkt. Hezron Makundi, Mhadhiri wa ChuoKikuu cha Dar es Salaam.

Diplomasia ya Uchumi niMkakati wa nchi kushirikiana na mataifa mengine, mashirika au taasisi zakimataifa kujinufaisha kiuchumi kupitia biashara, uwekezaji, utalii na teknolojia.

No comments:

Post a Comment