Saturday, 6 November 2021

IKUNGI WAPITISHA AZIMIO LA KUMPONGEZA MHE, RAIS SAMIA

 


Baraza la madiwani Halmashauri ya Wilaya ya ikungi leo katika kikao cha kawida cha baraza wamepitisha kwa kauli moja azimio kumpongeza Mhe Rais Samia Suluhu Hassan kufuatia Halmashauri hiyo kupewa zaidi ya shilingi Bilioni tatu ikiwa ni sehemu ya fedha zilizotolewa katika kupambana na Changamoto za UVIKO 19 Mwenyekiti wa baraza la madiwani Mhe Aliy Juma Mwanga akizungumza wakati wa kufungua kikao cha baraza amesema Halmashauri imepokea ya shilingi bilioni 2.6 fedha za ujenzi wa madarasa 67 mapya ya shule za secondary na madarasa 65 mapya ya shule shikizi za msingi na zaidi ya milioni 860 kwenye miradi ya maji Mhe Mwanga amesema fedha hizo ni nyingi ambazo zilikuwa nje ya bajeti ya Halmashauri na kwa pamoja wamemuomba Mkuu wa wilaya ya Ikungi Ndugu Jerry Muro ambae alikuwa mgeni rasmi kwenye kikao cha baraza kufikisha salamu na azimio la pongezi la madiwani kwa Mhe Rais, Samia Suluhu Hassan Akizungumza wakati wa kupokea azimio hilo, mkuu wa wilaya ya Ikungi Ndugu Jerry Muro amesema Serikali ya awamu ta sita itaendelea kupeleka fedha za miradi ya Maendeleo kama ambavyo imelekezwa katika ilani ya chama cha mapinduzi na kusisitiza kuwa Serikali itaendelea kutafuta vyanzo vipya vya fedha kwa ajili ya kuongeza wigo wa utoaji wa huduma za kijamii


Imetolewa na Halmashauri ya wilaya ya Ikungi

05/11/2021

No comments:

Post a Comment