Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Amos Makalla (katikati,) akiwa katika moja ya nyumba ya makazi 'Magomeni Kota' ambako alitembelea mradi huo uliokamilika kwa asilimia 99.


 MKUU Wa Mkoa wa Dar es Salaam Amos Makalla ameipongeza Wakala wa Majengo Tanzania (TBA,) kwa kusimamia vyema  mradi wa nyumba za makazi 'Magomeni Kota' mradi ambao umekamilika kwa asilimia 95 na jumla ya wakazi 644 waliokuwa wakiishi katika eneo hilo watarejea katika makazi hayo kama Ilivyohaidiwa na aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati John Joseph Magufuli.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam mara baada ya kutembelea mradi huo Makalla amesema, ameridhika na utekelezaji wa mradi huo ambao umekamilika kwa asilimia kubwa na kuwahakikishia wakazi 644 waliokuwa wakiishi hapo haki yao ya kurejea katika makazi hayo ipo palepale na kuwataka kujiepusha na matapeli wanaojifanya wafanyakazi wa Serikali na TBA na kuwataka kutoa fedha ili waweze kupangishwa nyumba hizo na kuviagiza vyombo vya ulinzi na usalama kuwasaka matapeli hao.

Amesema,katika makazi hayo hakuna nyumba zaidi za kupangisha  isipokuwa za wakazi 644 walioainishwa, upangaji utakaohusishwa watu wengine ni jengo la kitega uchumi yakiwemo maduka pindi litakapokamilika.

Aidha Makalla ameipongeza Serikali inayoongozwa na Rais Samia kwa kuahidi kutekeleza miradi yote iliyohaidiwa na mtangulizi wake na hadi sasa miradi hiyo ipo katika utekelezaji na kuishauri TBA kulitumia kimkakati eneo kubwa lililobaki katika makazi hayo.

Kwaupande wake Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Miliki Said Mndeme amesema, hadi sasa makazi yao yamekamilika na mchakato uliopo ni wa kuingiza umeme na tayari transifoma tano zimefungwa na zoezi hilo litakapokamilika hatua itakayofuata na kutoa semina elekezi kwa wapangaji 644 watakaoingia katika nyumba hizo.

Mndeme ameishukuru Serikali kwa kuendelea kuiamini Wakala hiyo katika usimamizi na utekelezaji wa miradi mbalimbali nchini.
Share To:

Post A Comment: