Kamishina wa Ushirikishwaji wa Jamii, Dkt Mussa Ali Mussa akishirikiana na vikundi vya sungusungu vya Buhulyo, Isagenhe na Zugimlole kucheza na kuimba nyimbo za kabila za kisukuma  jana katika Kata ya Isagenhe Tarafa ya Bukene Wilaya ya Nzega Mkoa wa Tabora ikiwa ni siku ya pili ya ziara yake ya ukaguzi wa uwepo wa Polisi Kata akishirikiana pia na taasisi ya Hans Seidel Foundation kutoa elimu kuhusu mpango wa Polisi Kata kama nynzo muhimu itakayosaidia kushughulika na kero za wananchi kuanzia ngazi ya Kata. Kamishna Dkt. Mussa na Taasisi ya Hans Seidel Foundation wametoa elimu hiyo kwa Kamati za Ulinzi na Usalama za Mkoa na Wilaya, Watendaji wa Kata na Vijiji pamoja, Kamati za Maendeleo za Mkoa na Wilaya pamoja na wananchi.
Kamishina wa Ushirikishwaji wa Jamii, Dkt Mussa Ali Mussa akizungumza na wananchi wa Kata ya Isagenhe Tarafa ya Bukene Wilaya ya Nzega ikiwa ni siku ya pili ya ziara yake ya ukaguzi wa uwepo wa Polisi Kata na kutoa elimu kuhusu Mpango wa Polisi Kata.
 
 Meneja Miradi wa Shirika la Hans Seidel Foundation (HSF) Kadele Mabumba akizungumza na wananchi wa ya Isagenhe Tarafa ya Bukene Wilaya ya Nzega Mkoa wa Tabora walipokua katika ziara ya Pamoja na Kamishna wa ushirikishwaji wa Jamii ya kutoa elimu kuhusu Mpango wa Polisi.
 
Kamishina wa Ushirikishwaji wa Jamii, Dkt Mussa Ali Mussa akimkabidhi Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Safia Jongo vitabu vya Mpango wa Polisi Kata Tanzania kwa ajili ya kuwakabidhi watendaji wa Kata wa Wilaya ya Nzega ili vitabu hivyo viwasaidie katika utekelezaji wa Mpango wa Polisi Kata. 
Askari wa Sungusungu vikundi vya Buhulyo, Isagenhe na Zugimlole wa Jamii ya kisukuma wa Kata ya Isagenhe Tarafa ya Bukene Wilaya ya Nzega wakiimba na kucheza jana wakati wa ziara ya Kamishina wa Ushirikishwaji wa Jamii, Dkt Mussa Ali Mussa alipowatembelea katika Kata hiyo ikiwa ni siku ya pili ya ziara yake ya ukaguzi wa uwepo wa Polisi Kata na kutoa elimu kuhusu Mpango wa Polisi Kata.
Share To:

Post A Comment: