Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Angeline Mabula, akizungumza katikati ya wiki na watumishi wa idara za ardhi na wadau mbalimbali wa Mkoa wa Singida katika ziara yake ya siku moja ya kukagua utendaji kazi wa sekta ya ardhi. Kutoka kulia ni Mwakilishi wa Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Singida Mjini, Eva Jeremia na Kamishna wa Ardhi Msaidizi Mkoa wa Singida, Shamim Hozza.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula (kulia) akingalia namna upimaji ardhi unavyofanyika kwa kutumia teknolojia ya kisasa katika Kijiji cha Mnang’ana wilayani Ikungi mkoani Singida alipokwenda katikati ya wiki kukagua mradi wa upimaji ardhi unaotekelezwa kwa pamoja na UN WOMEN, UNFPA na Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi kwa ufadhili wa KOICA. Kutoka kushoto ni Mpima Ardhi Arafat  Rajab, Kaimu Mkuu wa Idara ya Ardhi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi, Ambrose Ngonyani na Mpima Ardhi Aisha Juma.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula, akizungumza na wananchi na Wapima Ardhi wa Kijiji cha cha Mnang’ana.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula, akizungumza na watoto mapacha Hussein Yusuf (kushoto) na Hassan Yusuf ambao walikuwa katika zoezi la kupimiwa ardhi zao waliopatiwa na wazazi wao. Kulia ni Baba wa watoto hao Yusuf Misanga Diwani mstaafu wa Kata ya Sepuka.
Kaimu Mkuu wa Idara ya Ardhi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi, Ambrose Ngonyani (kushoto),akielezea zoezi la upimaji wa maeneo hayo. Kutoka kulia ni Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula, Kamishna wa Ardhi Msaidizi Mkoa wa Singida Shamim Hozza na Diwani wa Kata ya Sepuka, Halima Athuman Nyimba.
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula, akikabidhi hati za kiwanja.
Hati za viwanja zikikabidhiwa.
Father Manoel Tsing akizungumza kwenye kikao hicho.
Kikao kikiendelea.
Father Justine Boniface akizungumza kwenye kikao hicho.


Na Dotto Mwaibale, Singida.


NAIBU Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Angeline Mabula amekutana na wadaiwa sugu wa kodi ya pango la Ardhi Mkoa wa Singida ili kutafuta njia bora za kulipa madeni hayo.

Mabula alikutana na wadaiwa hao katikati ya wiki hii baada ya kukutanishwa nao kwenye kikao chake na watumishi wa idara za ardhi na wadau mbalimbali wakati wa ziara yake ya kikazi ya siku moja ya kukagua utendaji kazi wa sekta ya ardhi mkoani hapa.

Alisema kwenye Sheria ya ardhi kifungu cha (33) kifungu kidogo cha (3),kinasema mtu yeyote ambaye anamiliki ardhi anatakiwa kulipa kodi ya pango la ardhi kama sheria inavyoelekeza.

Alisema lakini kuna baadhi ya watu baada ya kupimiwa maeneo yao hujificha na  hawaendi kuomba kumilikishwa ili waanze kulipa kodi.

Alisema kutokana na hali hiyo Serikali iliona iweke utaratibu kwa  mtu yeyote ambaye amepimiwa eneo lake apewa siku 90 za kuomba kumilikishwa na asipofanya hivyo baada ya siku hizo atatakiwa kulipa kodi, ambapo pia ilitoa msamaha kwa waliopimiwa kipindi cha nyuma wataanza kulipa kuanzia mwaka jana sheria ilipoanzishwa.

Mabula alisema wizara imeamua kutoa nafasi hiyo kwa wadaiwa hao kabla ya kuanza utekelezaji wa sheria ili waweze kujua wajibu wao kama raia, taasisi na watu binafsi wa kulipa kodi ambapo wizara itatoa nafasi ya mwaka mmoja waweze kulipa madeni yao.

"Niwatake watumishi wa wizara hii mkaanze kusimamia sheria, kwasababu hamsimamii sheria vizuri ndio maana mchakato huu wa kulipa kodi unakuwa mgumu,nniwaombe walipa kodi lipeni kodi zenu kila mwaka mkivusha zoezi la kulipa litakuwa zito kwasababu kiwango kitaongezeka kutokana na kulimbikiza." alisema Mabula.

 Kamishna wa Ardhi Msaidizi Mkoa wa Singida Shamim Hozza akisoma taarifa ya utekelezaji wa wizara hiyo mkoani hapa alisema mkoa ulipangiwa kukusanya maduhuri yatokanayo na ardhi Sh. Bilioni moja na milioni mia tisa lakini walikusanya Sh. Bilioni moja na milioni mia mbili sawa na 66%.

 Alisema moja ya changamoto zilizosababisha ofisi yake kushindwa kufikia lengo ni madeni makubwa ya Serikali na baadhi ya taasisi za dini ambazo zimekuwa na ukakasi wa kulipa madeni hayo.

Hozza  alisema ili kukabiliana na changamoto hizo ofisi yake inaendelea kufanya jitihada mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuhamasisha na kufanya mikutano ya wananchi pamoja na kutoa matangazo kwa njia mbalimbali, kutoa nyaraka za umilikishaji na madeni na kwa wale ambao walikaidi kulipa madeni walifikishwa kwenye mabaraza ya ardhi kwa hatua zaidi.

Dkt.Mabula kabla ya kufanya kikao hicho alishiriki katika zoezi la mradi wa upimaji mipaka ya vijiji na makazi katika Kijiji cha Mnang'ana wilayani Ikungi ambao unatekelezwa kwa pamoja na mashirika ya UN WOMEN, UNFPA na Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi kwa ufadhili wa KOICA.

Share To:

Post A Comment: