Mbunge wa jimbo la Ludewa Joseph Kamonga (kulia) akipokea zawadi ya mbuzi kutoka kwa wananchi wa kijiji cha Mavanga.
Baadhi ya wananchi wa kijiji cha Mavanga wakimlaki mbunge wao Joseph Kamonga baada ya kuwasili Kijiji hapo.
Mbunge wa jimbo la Ludewa Joseph Kamonga akiwagawia gazeti la mwananchi wakazi wa kijiji cha Mavanga ambalo ndani yake kuna makala iliyohusisha kijiji hicho.
Wananchi wa kitongoji cha Luhuhu getini wakiwa wamejiandaa na zawadi zao tayari kwa kumkabidhi mbunge wa jimbo la Ludewa Joseph Kamonga (kulia)
Mbunge wa jimbo la Ludewa Joseph Kamonga (kulia) akipiga ngoma huku wananchi wakiselebuka baada ya kuwasili kitongoji cha Luhuhu getini
Mbunge wa jimbo la Ludewa Joseph Kamonga (aliyevaa suti) akiburudika pamoja na kikundi cha ngoma.
Mbunge wa jimbo la Ludewa Joseph Kamonga (kushoto) wakijadiliana jambo na viongozi wenzake. Anayefuata ni Diwani wa kata ya Mavanga Daudi Luoga na katibu wa mbunge huyo Alphonce Mwapinga.
Wakazi
wa kata ya Mavanga iliyopo wiliya ya Ludewa mkoani Njombe
wamewalalamikia walimu wakuu pamoja na Afisa elimu wa kata hiyo kwa
kuwalazimisha kulipia fedha kwa mtoto atakayeshindwa kufika shuleni
pamoja na kuwalipa walimu wa kujitolea.
Wakitoa malalamiko hayo
mbele ya mbunge wa jimbo la Ludewa Joseph Kamonga alipofanya ziara
katika kijiji cha Mavanga, Mbugani pamoja na kitongoji cha Luhuhu getini
wananchi hao wamedai kuwa walimu hao wamekuwa wakiwatoza kiasi cha
shilingi elfu tano kwa siku na endapo mwanafunzi hatofika shuleni siku
tano basi wanatakiwa kulipa elfu 25,000.
Melania Mtweve ni mmoja
wa wananchi hao ambaye ni mkazi wa kijiji cha Mavanga amesema
wanashindwa kuelewa hizo fedha wanazitoa kwa malengo gani kwani
wasipolipa watoto hurudishwa nyumbani mpaka aende na hiyo fedha.
"
Kwa elimu ya mtindo huu ni bora watoto wangu wakaage nyumbani maana
shule sasa hivi imekuwa ni mradi unaojitegemea ambao unawanufaisha
walimu kwasababu mara nyingine mtoto anashinda shule kwa mambo ya msingi
si kwa makusudi", Alisema Mtweve.
Sanjari na suala hilo pia
wazazi hao wameiomba serikali kuajili walimu wa kutosha kwani wamekuwa
wakilazimishwa kuchangia kiasi cha shilingi elfu 10,000 kwa kila
mwanafunzi ili kuwalipa walimu wanaojitolea.
Akizungumza hayo
mmoja wa wakazi wa kitongoji cha Luhuhu getini David Mgaya amesema kuwa
michango hiyo inawapa tabu sana kwani endapo mzazi anakuwa na watoto
watano analazimika kulipa elfu 50, 000.
Mgaya ameiomba serikali
kulichukulia suala hilo kwa uzito kwani wananchi wanahali ngumu na
wanaposhindwa kulipa fedha hizo walimu wamekuwa wakiwasumbua watoto
mashuleni ikiwemo kuwakamata wazazi na kuwapeleka katika ofisi za
kijiji.
Akijibu hoja hizo afisa elimu wa kata hiyo Hosea Chaula
amekiri kuwepo kwa malipo hayo ya kutofika shuleni na kuwalipa walimu wa
kujitolea na kudai kuwa hayo yote yanatekelezwa kwa makubaliano kati ya
kamati ya shule na wazazi.
Ameongeza kuwa wazazi na kamati hiyo
ilikubaluana kuwalipisha fedha endapo watoto hawatafika shuleni ili
kukomesha tabia za utoro kwa wanafunzia hao na kuwafanya wazazi wawe
wanawahimiza watoto kufika shule.
Amesema kwa upande wa kuwalipa
walimu wa kujitolea ni njia mojawapo ya kuwasaidia wanafunzi kupata
elimu bora kutokana na uhaba wa walimu huku akitoa mfano wa shule ya
msingi Ushindi ambayo ina wanafunzi 436 huku walimu walioajiliwa wakiwa
sita hivyo wamelazimika kuongeza walimu wawili ambao hulipwa na wazazi
hao.
"Haya yote tunatekeleza kwa mujibu wa makubaliano na wazazi
na kwakuwa ni makubaliano nasi tunahakikisha tunafuatilia michango yote
ambapo fedha ya walimu wa kujitolea hulipwa kwa awamu tatu kwa mwaka
mwezi wa tatu, saba na tisa", Alisema Chaula.
Aidha kwa upande wa
mbunge wa jimbo la Ludewa Joseph Kamonga amewataka viongozi hao wa
elimu kufuata utaratibu wa utungaji sheria ndogo ndogo ambapo zinatakiwa
kupitishwa na baraza la madiwani kwani ukusanyaji wa fedha kiholela ni
sawa na kuiba.
Amesema kila malipo yaliyo halali yanapaswa
kukatiwa risiti hivyo kama kunaulazima wa kutoza faini kwa mtoto
asiyefika shule basi wapitishe sheria hiyo na wananchi wapewe risiti
wafanyapo malipo hayo ikiwezekana ijulikane fedha hizo zinapikwenda.
Ameongeza
kuwa suala la wazazi kuajili walimu hata bungeni amewahi kulizungumzia
sambamba na kuiomba serikali kuleta walimu ambapo mpaka sasa tayari
walimu 140 wameajiliwa wilayani Ludewa na bado anaendelea kupambana ili
kupata walimu wengine zaidi.Hata hivyo amesema kuwa fedha hizo
wanazotozwa wazazi kwaajili ya kuwalipa walimu wa kujitolea ni nyingi
sana hivyo wanapaswa kupunguza kiwango cha malipo hayo.
"Nikweli
serikali ina wajibu wa kuajili walimu lakini pia kwa nafasi yangu
nitaendelea kuishauri serikali iajili walimu hao wanaojitolea ili waweze
kuwa wakudumu na kuingizwa katika mfumo na hiyo ya kutofika shule
kuanzia leo naizika haitakuwepo tena kama watawadai waambieni waje
wachukue kwangu na mnapokuja kwangu hakikisheni mnanipa na risiti",
Alisema Kamonga.
Post A Comment: