Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. John Mongela,amewataka Wananchi wa Mkoa huo kuepuka mikusanyiko isiyo ya lazima sambamba na kuendelea kuchukua tahadhari ya ugonjwa wa UVIKO-19 kwa kuvaa barakoa na kunawa mikono kwa sabuni na maji tiririka.
Mhe.Mongela
 ameagiza hayo wakati wa ziara yake  ya siku moja  Wilayani Arumeru ya 
kukagua mashamba ya mazao ya mbogamboga, maua, matunda na viungo kwa 
lengo la kuona uhalisia wa uendeshaji wa mashamba hayo.
	
Aidha,
 amesema   Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Mhe.Samia Suluhu Hassan, 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inaendelea kuhakikisha  sekta 
zote za kiuchumi zinakuwa na tija.
	
Mhe.Mongela
 amesema baada ya kutembelea mashamba hayo siku ya Kesho atakua na kikao
 na wadau wa Kilimo cha mazao ya mbogamboga, matunda na maua ili 
kuhakikisha sekta hiyo inafanya vizuri.
	

Post A Comment: