Wednesday, 21 July 2021

MATAMASHA MAWILI YA FALLY IPUPA YAAHIRISHWA, MASHABIKI WAOMBWA RADHI

 

MENEJIMENTI ya mkali wa Rhumba Afrika, Fally Ipupa imetangaza kuahirisha Matamasha mawili ya msanii huyo yaliyokua yafanyike Ijumaa ya Julai 23 na Jumamosi ya Julai 24 mwaka huu.

Kwa mujibu wa taarifa iliyoolewa na uongozi wa msanii huo kampuni ya Prime Time Promotions inasema ahirisho la matamasha hayo mawili yaliyokua yafanyike jijini Dar es Salaam katika Hoteli ya Serena na jijini Mwanza katika Hotel ya Elevate Malaika yameahirishwa kutokana na changamoto zilizoshindwa kuepukika.

Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya matamasha hayo, Edward Lusala ameomba radhi kwa mashabiki wa muziki na msanii huyo nchini huku akieleza kuwa utaratibu kwa walionunua tiketi tayari utatolewa.

" Menejimenti ya Fally Ipupa, Prime Time Promotion na Clouds Media Group inachukua nafasi hii kuomba radhi kwa wale wote ambao walikua wametenga ratiba yao ili kuwa sehemu ya matukio haya. Tarehe mpya za show zitatangazwa baadae.

Utaratibu kwa walionunua tiketi na kufanya booking ya meza utafafanuliwa kwa mawasiliano kati yao na kamati husika," Amesema Lusala.

No comments:

Post a Comment