Katibu Mkuu wa Uchukuzi Bw, Gabriel Migire akifungua Mkutano wa 26 wa Baraza Kuu la Wafanyakazi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania katika Ukumbi wa PSSSF Jijini Dar Es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania Mhandisi Mshauri Julius Ndyamukama alipokuwa akisoma taarifa ya utendaji wa Mamlaka kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi kwaajili ya ufunguzi wa Mkutano 26 wa Baraza Kuu la Wafanyakazi uliofanyika katika  Ukumbi wa PSSSF Jijini  Dar Es Salaam.
Baadhi ya wajumbe kutoka Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania walioshiriki katika Mkutano wa 26 wa Baraza Kuu la Wafanyakazi uliofanyika katika  Ukumbi wa PSSSF Jijini  Dar Es Salaam.
Kaimu Mkurugenzi wa Fedha na Biashara CPA Shedrack  Chilongani aliesimama akiwasilisha mpango mkakati wa TAA wa mwaka 2021/2022 - 2025/2026   kwa wajumbe wa Baraza wakati wa  Mkutano  wa 26 wa Baraza Kuu la Wafanyakazi uliofanyika katika  Ukumbi wa PSSSF Jijini  Dar Es Salaam .
Katibu Mkuu Uchukuzi Bw, Gabriel Migire (katikati)akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa walioshiriki katika Mkutano wa 26 wa Baraza Kuu la Wafanyakazi uliofanyika katika  Ukumbi wa PSSSF Jijini  Dar Es Salaam( tatu toka kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya ndege Tanzania Mhandisi Mshauri Julius Ndyamukama.


Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi, (Sekta ya Uchukuzi)  Bw, Gabriel Migire amewataka wafanyakazi wa TAA kuhakikisha wanatumia  rasilimali vizuri kulingana na sheria , miongozo na taratibu zilizopo  ili kuondoa  hoja za ukaguzi zinazoweza kutokea. 

 Bw, Migire alisema hayo  alipokuwa akifungua mkutano wa 26 wa Baraza Kuu la Wafanyakazi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Dk. Leonard Chamuriho katika ukumbi uliopo katika jengo la PSSSF Jijini Dar  Es- Salaam.

 “Wafanyakazi wa umma wanapaswa kuhakikisha wanafanya matumizi mazuri ya rasilimali zilizopo ili kuondoa   hoja za ukaguzi , watumishi  mnapaswa kufanya yale ya msingi yanayotarajiwa  na wadau mbalimbali  hata wa Kimataifa  na pia  mhakikishe Taasisi ina jina zuri kutokana na utendaji kazi wenu" amesema Bw, Migire. 

 Akizungumzia  Mpango Mkakati wa mwaka 2021/2022 - 2025/2026 na bajeti ya mwaka 2021/2022 ya TAA iliyowasilishwa katika baraza hilo, Bw. Migire alisema,  katika maandalizi ya bajeti na Mpango Mkakati ni vema kuweka  misingi ambayo itawezesha mambo mengine yote ya kiutendaji  yaende vizuri na baadae kufanyiwa tathmini ya namna ya utekelezaji wake. 

 Aidha alisisitiza kuwa mipango ya Taasisi  si ya viongozi tu bali ni ya watumishi  wote kwa pamoja na bila hivyo ni kupoteza muda na rasilimali fedha za umma.

Hata hivyo, Bw, Migire amesema ni imani yake kuwa  maandalizi hayo ya bajeti  yalienda kwa kufuata miongozo iliyowekwa   na kuhakikisha agenda za Kitaifa zinatafsiriwa vema  katika maeneo ya kazi huku akiwataka wajumbe waelewe vizuri bajeti hiyo na kwenda kuitekeleza na kutenda haki maana bajeti ni takwa la kisheri. 

Awali akimkaribisha Bw. Migire Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania Mhandisi Mshauri Julius Ndyamukama alisema, Ufanisi wa Mamlaka  katika kipindi cha miaka ishirini na moja iliyopita umekuwa ni wa kuridhisha kutokana na maboresho ya miundombinu ,  ununuzi wa vifaa vya uendeshaji na ubora wa huduma huku  mapato yakiwa yameongezeka kutoka bilioni 4.2 kwa mwaka 1999/2000 hadi kufikia shilingi bilioni 101.4 kwa mwaka 2019/2020.

  Vilevile, TAA imefanikiwa kuthibitishwa katika ISO katika maeneo matatu ya ithibati, ambayo ni ISO 9001:2015; 14001:2015 na 45001:2018) ya Quality Management System: Environment Management System: Occupational Health and Safety System.

 Kwa upande mwingine,  Mhandisi Ndyamukama alisema TAA inakabiliwa na baadhi ya Changamoto ikiwemo ya upungufu wa Wafanyakazi na gharama kubwa za utwaaji na umiliki wa maeneo  ya Viwanja vya ndege huku akiiomba Wizara kuweza kusaidia katika  changamoto hizo.

 Mkutano huo wa 26 wa Baraza Kuu la Wafanyakazi unafanyika kwa  siku mbili kuanzia Tarehe 7- 8 Mei 2021 katika Ukumbi uliopo Jengo la PSSSF, Jijini Dar Es Salaam ukijumuisha Wajumbe Kutoka Kanda mbalimbali za TAA nchi nzima na unatarajiwa kufungwa  tarehe 8 Mei, 2021.

Share To:

TANZANIA YA KIJANI

Post A Comment: