Angela Msimbira TAMISEMI


Kamati ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa imeshauri Serikali kudhibiti madalali katika upatikanaji wa vizimba na ushushaji wa mizigo katika soko la kisasa la Ndugai jijini Dodoma.


Kamati imetoa ushauri  huo mara baada ya ziara ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa walipotembelea soko la Ndugai kuangalia hali ya utoaji wa huduma Katika soko hilo ambalo limejengwa na Serikali kwa gharama ya Sh bilioni 14.6.


Akizungumza katika ziara hiyo Mbunge wa Hai Mhe. Saasisha Mafuwe amesema kushindwa kuimarika kwa biashara katika soko hilo kunatokana na madalali kuhodhi vizimba sambamba na kuzuia magari ya mizigo kushusha hapo. 


Aidha skichangia hoja katika Soko hilo hMbunge wa Viti Maalum(CCM) Balozi Pindi Chana amewataka wataalam kuahkikisha wanafanya utafiti wa kupata takwimu sahihi ya wafanyabiashara wanaotumia soko hilo na kuwahamasaisha wananchi kujenga  katika eneo hilo ili Soko liweze kuchangamka na kuwavutia wananchi kuja kununua bidhaa katika Soko hilo.


Akihitimisha katika ziara hiyo Makamu Mwenyekiti wa Kamati Mhe. Chaurembo  kusema kuwa miradi ya ujenzi wa masoko katika Halmashauri izingatie mahitaji ya wananchi kwa kuwa mengi hujengwa kwenye maeneo ambayo uendeshaji wake umekua mgumu na kufanya miradi hiyo kutokuingiza mapato kwa Serikali.


Mhe. Abdallah Chaurembo ameshauri kuhakikisha  mikakati endelevu ya kutoa elimu kwa jamii inawekwa ili kuwajengea wananchi uelewa kuhusu matumizi ya masoko nchini 


“Wananchi wengi wamekuwa wakiogopa kuingia kwenye masoko yaliyojengwa kwa kuhofia gharama ya vitu kuwa kubwa hivyo Serikali iweke mikakati ya kutoa elimu ili kuondoa dhana hiyo” Amesisitiza  Mhe. Chaurembo.


Akijibu hoja za Wabunge Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Ummy Mwalimu ameieleza Kamati kuwa watahakikisha wanafanya mapitio ya  mpango wa biashara wa soko la Ndungai  ili uendane na  kile kilichokusudiwa.


Mhe. Ummy amefafanua  kuwa ili kuweza kurejesha uwekezaji wa shilingi  bilioni 14.6  kuna haja ya kupitia mpango wa  biashara wa kuanzishwa kwa soko hilo ili isiende kinyume na matarajio yaliyopangwa awali


Mhe. Ummy amesema  kuwa Serikali itakuja na mkakati wa kutekeleza maoni  na ushauri walioutoa wajumbe wa kamati hiyo ambao utasaidia kuboresha utoaji wa huduma katika Soko hilo la Kisasa.


“ Mradi wa Soko la Ndigai ulibuniwa kwa kuangalia « Long tame plan » kwa kuwa Dodoma imekuwa ni Makao Makuu ya Nchi, lakini pia ongezeko la watu , hivyo ni kweli zimewekwa  shilingi bilioni 14.6 lakini ukiangalia  makisio ya marejesho kiasi hicho cha Fedha kitarudi” amesema Mhe. Ummy


Amesema kuwa kwa mwaka  ilikadiriwa kupata kiasi cha shilingi  bilioni 1.8   hivyo kwa muda wa miaka 15 itawezekana kupata shilingi bilioni 27 na tangu soko limeanza kufanya kazi tayari wameshakusanya kiasi cha shilingi milioni 100 hivyo  mpango wa muda mrefu utalipa.


Mhe. Ummy amesema kuwa viwanja vingi vya makazi vimetengwa mtumba , nzuguni , Chamwino ambapo bado hapajajengwa hivyo wanategemea mara baada ya watu kujenga watakuwa wakitumia soko hilo kupata huduma za mahitaji mbalimbali ya kijamii.

 

Aidha Ameuelekeza  Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa kuhakikisha wanapitia mpango wa biashara wa  Soko la Ndugai ili liendane na  uhalisia wa awali nini kilikuwa kimekusudiwa katika soko hilo.


Aidha amewagiza Halmashauri ya Jiji la Dodoma kuhakikisha wanawaondoa madalali katika soko hilo kwa kufanya  utafiti wa kina wamiliki wa vizimba  ili kuwa na wamiliki halali wa maeneo yao.

Share To:

msumbanews

Post A Comment: