Na Woinde Shizza, ARUMERU

Hali ya Taharuki imewakumba wananchi wa Vijiji vya Embaseni na Maji ya chai wilayani Arumeru Mkoani Hapa ,kufuatia mnyama aina ya kiboko kuvamia makazi yao na kuwajeruhi watu wawili  na kujaribu pikipiki.

Hata hivyo Kiboko huyo aliuawa na askari wa wanyama pori na wananchi wa vijiji hivyo  kugombania Nyama yake kwa kugawana mapande ya nyama wakiwa na visu,Mapanga na Sime.

Kiboko huyo anayedaiwa kutoroka kutoka hifadhi ya Taifa ya Arusha ANAPA ,na kuzua taharuki katika vijiji hivyo mapema jana majira ya asubuhi pale alipoibuka  ghafla na kushambulia wakazi wawili ambao hali zao zitaendelea vizuri.

Kwa mujibu wa mwenyekiti wa Kijiji cha Maji ya Chai ,David Mbise mnyama huyo alionekana akizunguka katika Kijiji hicho Jana asubuhi hata hivyo watu walianza kumzonga kwa kufuata nyuma kila napokwenda ndio alipopandwa na hasira na kuwafukuza watu aliokutana nao mbele yake na kuwajeruhi wawili. 

"Wakati watu wakimfuatilia ndipo alimkamata mtu mmoja na kumng'ata hadi kumvunja mguu na mwingine alimng'ata mgongoni na baadaye aliikuta pikipiki yangu imeengeshwa ambapo nayo aliing'ata na kuiharibu alisema shuhuda.

Naye mwenyekiti wa Kijiji Cha Embaseni Joshua Nasari alisema kuwa Mara baada ya mnyama kujeruhi watu katika Kijiji Cha Maji ya chai alikiambia na kuvuka mto na kuingia katika Kijiji chake lakini hakuwez kujeruhi mtu yeyote lakini Askari wa wanyama pori walifanikiwa kumuua .

Baadhi ya wananchi wa vijiji hivyo walionufaika na Nyama ya Kiboko baada hiyo ,Daruweshi Abdala alisema kuwa hakuwahi kula nyama ya kiboko Ia ujio wake  kumesababisha kupata kitoweo ambacho hakukitarajia.

Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Arumeru Jerry Muro ambaye Ni mwenyekiti wa ulinzi na usalama wilaya ya Arumeru alithibitisha kujeruhiwa kwa watu wawili akiwemo mmoja kuvunjwa mkuu.

Alisema Mara baada ya kupata taarifa alifika eneo la tukio na kushuhudia majeruhi hao huku majeruji mwingine akiwa amejeruhiwa eneo la ubavuni.

Hata hivyo Muro aliwasihi wananchi hao kuchukua tahadhari kutokana na wanyama hao kuvamia maeneo ya makazi kwa kutoa taarifa mapema kwa vyombo husika ili hatua za haraka ziweze kuchukuliwa.

Aidha alizitaka mamlaka.husika ikiwemo hifadhi za Taifa Tanapa kuona umuhimu wa kugharamia matibabu ya wahanga wa wanyama hao kwa haraka zaidi na kuona namna ya haraka ya kuwalipa kifuta jasho.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: