Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amemsimamisha kazi Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari nchini TPA Mhandisi Deusdedit Kakoko, kupisha uchunguzi wa ubadhirifu wa fedha bandarini.

Rais Samia amefikia uamuzi huo leo Jumapili, Machi 28, 2021 baada ya ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) na Takukuru Ikulu ya Chamwino, Dodoma.

“Ripoti nimeona, nimeipitia na nimebaini ubadhirifu mkubwa uliofanywa pale bandari, hili suala mnatakiwa kushirikiana, nakuomba Takukuru jishughulishe pale, alipita Waziri Mkuu alilishughulikia.

“Waziri Mkuu aliunda kamati na wakafanya uchunguzi kidogo ambao yaliyotoka, hatua chache zilichukuliwa lakini imani yangu ni kwamba kama kuna ubadhirifu pale waliosimamishwa ni hawa wa chini huku, ninaomba mara moja nitoe agizo la kumsimamisha Mkurugenzi Mkuu wa Bandari halafu hatua zaidi ziendelee,” amesema Rais Samia.

Share To:

Post A Comment: