MCHIMBAJI mdogo wa madini ya rubi katika Kata ya Mundarara wilayani Longido mkoani Arusha, Sendeu Laizer ambaye alibuka na utajiri katika sekta hiyo baada kupata tani tano za madini hayo zenye thamani ya zaidi ya Shilingi bilioni 1.7 ameishukuru serikali kupitia wizara ya madini pamoja na tume ya madini kwakutambua mchango wake katika sekta ya madini.

Akizungumza na waandishi wa habari leo mkoani hapa , Gabriel Sendeu Laizer alisema kuwa ameishukuru serikali kutambua kazi anayoifanya na kumpa cheti cha kutambua mchango wake pamoja na zawadi ,alizopewa katika mkutano wa kimataifa wa uwekezaji katika sekta ya madini 2021 mkutano uliofanyika katika kituo cha mikutano cha kimataifa cha Julius Nyerere.

Aliishukuru serikali na kusema kuwa mafanikio aliyoyapata ni matokeo ya hatua zinazochukuliwa na serikali ya kuwajengea wachimbaji wadogo mazingira mazuri ya uchimbaji.

Aidha pia aliishukuru sekta ya madini na serikali hususani Rais John Magufuli kwa kuwathamini wachimbaji wadogo na kuwatetea hatua ambayo ndio iliyochangia mafanikio yake kwa sasa na sio vinginevyo.

Pia aliwashauri wachimbaji wenzake wadogo wa madini kuendelea kuchimba bila kukata tamaa kwani kazi hiyo inahitaji uvumilivu na kujitoa kwa Aidha aliwataka wachimbaji wenzake kuendelea kutoa ushirikiano kwa serikali ukiwemo kudhibiti utoroshaji wa madini ili yaendeleee kuwanufaisha wananchi na taifa kwa ujumla.

Share To:

Post A Comment: