NA HERI SHAABAN, (ZANZIBAR) 



MBUNGE wa Viti Maalum Mkoa wa Kaskazini Unguja, Bi . Angelina Malembeka amekabidhi pikipiki 12 kwa Masheha wa Sheiha 10 za  Mkoa huo Pamoja na pikipiki 2 kwa waratibu wa mbunge wa  Mkoa  huo ili kuweza kuendeleza kuwarahisishia kazi.


Akizungumza mara baada ya kukabidhi pikipiki hizo alisema kuwa utoaji wa pikipiki hizo umekuja kutokana na changamoto zilizojitokeza za upatikanaji wa Taarifa  mbalimbali wakati wa  kampeni kuwa hazifiki  kwa wakati.



Pikipiki hizo zimetolewa mapema leo hii  katika Viwanja  vya  Ofisi  ya  CCM Mkoa wa  Kaskazini  Unguja,ambapo tano zilitolewa kwa masheha wa Wilaya ya Kaskazini 'A' na Wilaya ya Kaskazini 'B' ambapo maeneo yao ni makubwa na hawana vitendea kazi.


"Tunapohitaji taarifa zinazohusu shehia zao huwa zinachelewa au zimekuja bila ya uhalisia hivyo mategemeo yetu pikipiki hizi zitatufanya tupate taarifa kwa wakati zinazohusu chama na huduma za kijamii i" alisema Malembeka .


Sambamba na hayo, alisema kuwa pikipiki hizo zitawapa nafasi za kufanya kazi na kupeleka kupata taarifa kwa wakati sambamba na kujenga mahusiano baina ya viongozi wa Chama na serikali.


"Masheha ni viongozi wa Serikali hivyo itaweza kuwasaidia wananchi kwa ukaribu zaidi kwani masheha ni viongozi wa Serikali nasi tunawasaidia  katika kufanya kazi kwa ufanisi zaidi" alisema.


Hata hivyo, aliwataka masheha hao kuzitumia kwa uangalifu kwa kuvaa kofia za kukinga Licha (Helmet) pamoja na kwenda kwa mwendo wa kawaida ili kuweza kuepusha ajali zilizokuwa sio za lazima pamoja na kufata sheria za barabarani ili kuepuka ajali zinazoweza kuepukika.


Naye, Mwenyekiti wa Wanawake Mkoa wa Kaskazini Unguja, Maryam Muharami Shomari, alisema kutolewa kwa pikipiki hizo, zinaonesha wazi kuwa mbunge huyo anatambua umuhimu wa masheha kwani kumekuwepo kwa umuhimu wa sheha katika kufanya kazi zao kwa umakini.


Maryam aliwataka wabunge wengine kuendeleza aliyoyaanza mbunge huyo ili kuweza kukamilisha idadi ya masheha waliokuwepo katika Mkoa huo kupata vitendea kazi katika Mkoa na wilaya zao.


Wakitoa shukrani kwa kupatiwa pikipiki hizo, sheha wa shehia ya Matemwe, Vuai Faraji Mcha, alisema ni Jambo la faraja kupatiwa pikipiki hizo na kuahidi kuitumia pikipiki hizo kuwa lengo lilokusudiwa ili kuona hali ya kiutendaji inakwenda kama ilivyopangwa pamoja na kumuahidi mbunge huyo kufanya kazi kwa lengo la kupatiwa.


Share To:

msumbanews

Post A Comment: