NA MWANDISHI WETU, CHALINZE.

 

MBUNGE wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete ameahidi kushughulikia kero mbalimbali ikiwemo ya barabara na daraja katika Kitongoji cha Msolwa, kilichopo Kata ya Bulingu, Jimboni humo.


Ridhiwani Kikwete ameaahidi hayo wakati wa ziara yake maalum ya kushukuru na kusikiliza kero za Wananchi hao kwa kukichagua kura nyingi Chama Cha Mapinduzi CCM ikiwemo kumpatia asilimia 90 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli.


Awali akipokea kero hizo kutoka kwa Wananchi, ikiwemo za ubovu wa barabara na daraja ambacho kimekuwa kilio kwa muda mrefu,


Wananchi hao walieleza kuwa, barabara hiyo imekuwa msaada mkubwa kwao hivyo wameomba matengenezo ilikupitika wakati wote ikiwemo kuwekewa daraja kwenye mto Mbiki


"Shida kubwa barabara yetu ya Makondo mengi ambayo imekuwa kiunganishi kwa wakazi wa vitongoji vya Msolwa na Makondo mengi pamoja na Vitongoji jirani wakati wa mvua ni kero kubwa  hata mazao yetu tunashindwa kusafirisha." Alieleza Devis Tema mkazi wa Bomani.


Mbali na barabara hiyo, pia Wananchi hao waliomba kujengewa daraja eneo la Mto Mbiki ilikuunganisha Makondo mengi na Bomani ilikuondoa kero za muda mrefu.


"Mto Mbiki ukijaa shughuli za kijamii zinasimama na wakati mwingine hata Wanafunzi kushindwa kwenda shule." Walieleza Wananchi hao.


Kwa upande wake, Mbunge Ridhiwani ambaye pia aliongozana na Wakuu wa Idara mbalimbali za Halmashauri hiyo akiwemo Mhandisi wa Halmashauri,  Mganga Mkuu, Kamanda wa TAKUKURU, Diwani wa Kata ya Buringu pamoja na viongozi wengine wa siasa alieleza:


"Ningependa sana kutumia nafasi hii kuwashukuru tena kwa kutuchagua.


Ujio wangu kwenu pia kupokea kero na maoni yenu kwa namna ya kuyapatia ufumbuzi. 

Kero mlizozieleza hapa mimi nimezipokea zote kwa heshima. Ninawahakikishia daraja lazima lijengwe." Alisema Ridhiwani Kikwete. 


Aidha, kuhusu barabara amesema Mhandisi tayari amejionea hali halisi lakini pia suala hilo ataliwasilisha TARURA kwa hatua zaidi.


Aidha, kero zingine Wananchi hao walizitoa kwenye mkutano huo, ni pamoja na mgogoro wa ardhi kati ya Wakulima na Wafugaji lakini pia suala la kuhitaji kujengewa Zahanati lakini pia kujengwa kwa shule ya Secondari Kitongoji cha Msolwa.

Share To:

msumbanews

Post A Comment: