Mbunge wa Arusha Mjini Mrisho Gambo akihutubia maelfu ya wananchi kwenye Soko kuu Jijini Arusha leo Mei 10, 2025.Amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa hatua yake ya kuufungua utalii Mkoani Arusha pamoja na mikutano mbalimbali, akieleza suala hilo limechangia kukua kwa uchumi wa mtu mmoja mmoja na wa mkoa kwa ujumla pamoja na kutoa ajira kwa wananchi wa Mkoa wa Arusha.
Mhe Gambo kadhalika ameeleza kuwa serikali ya Rais Samia ndani ya miaka minne ya uongozi wake, ameonesha dhamira ya kuzijenga barabara za Arusha pamoja na miundombinu mingine ya usafiri na usafirishaji ikiwemo uwanja wa ndege wa Arusha, akisema mambo hayo ndiyo yanayowafanya kuamua kumpa tena miaka mitano Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Awali Mbunge huyo pia ameshukuriwa na Madiwani wa Halmashauri ya Jiji kwa msukumo wake Mkubwa Bungeni katika kusema kero na changamoto za wananchi, wakiwasihi wananchi wa Arusha Mjini kutofanya Makosa wakati wa Uchaguzi Mkuu wa Oktoba mwaka huu.
Post A Comment: