Tuesday, 3 November 2020

AMBONI CAVES MARATHON 2020 KUTIMUA VUMBI FEBRUARY 7,2021

 


NA MWANDISHI WETU,TANGA.

MASHINDANO ya Riadhaa ya Amboni Caves Marathon 2020 yanatarajiwa kuanza kutimua vumbi February 7 mwakani na itashirikisha wakimbiaji kutoka maeneo mbalimbali ndani na nje ya nchi.

Akizungumza leo na Msumba News Blog Muandaaji wa Mashindano hayo Sophia Mura ambaye ni Mkurugenzi wa Kali Amboni Caves Tanga alisema maandalizi yanaendelea vizuri na wanatagemea kupata idadi kubwa ya washiriki.

Alisema kwamba malengo la kuandaa mashindano hayo ni kukimbia na kutangaza utalii wa ndani hususani katika maeneo ya mali kale ikiwemo Mapango ya Amboni na Tongoni ikiwem vivutio vyengine vilivyopo mkoani hapa

Muandaaji huyo alisema lengo la pili ni kutaka kuinua vipaji vya wakimbiaji wa ridhaa Jijini Tanga na kuvitangaza vionekane hatua ambayo itawawezesha kupata fursa mbalimbali kupitia mchezo huo.

“Lakini tutaendelea kuandaa na kushirikiana na chama cha riadhaa kuibua vipaji pamoja na kutangaza vivutio vya utalii vilivyopo mkoani Tanga kila mwaka “Alisema

“Nilipata wazo la kuanzisha marathoni hii kufanya utalii wa ndani kwa sababu Tanga kuna vivutio vingi vya utalii watakinmbia hapa mjini watapita kwenye maeneo mbalimbali na baadae watakwenda kutembelea kwenye vivutio hivyo”Alisema

Muandaaji huyo alisema madhumuni yake makubwa kuanzisha mashindano hayo ni kuinua vipaji vya wakimbiaji wa Jiji hilo la Tanga ili viweze kuendelezwa na kuonekana hatua itakayo wawezesha kutimiza ndoto zao.

Awali akizungumza Katibu wa Chama cha Riadhaa Mkoa wa Tanga Hassani Mwagomba alisema kwamba wamepata vibali vyote husika kuoka BMT wamesajiliwa kisheria na wamepata usajili kutoka Brela ikiwemo Baraka za Chama cha Riadha Tanzania.

Mwagomba ambaye pia ni Meneja wa mbio hizo alisema pia wamepata Baraka kutoka kwenye chama cha Riadhaa Mkoa wa Tanga huku akieleza kwamba wakiambiaji wote siku mbili 

Mashindano hayo yatakuwa na umbali wa kilomita 21,10 ,5 na 2.5 kwa ajili ya watoto,baada ya kumalziika mbio hizo watakuwa na fursa ya kwenda kufanya utalii kwenye mapango ya amboni kabla ya mashindano watawapimwa .

No comments:

Post a Comment