Monday, 19 October 2020

SEKONDARI YA MKWESE MANYONI MKOANI SINGIDA KUANZA KUTOA ELIMU YA STADI ZA UFUNDIWahitimu wa Kidato cha  Nne wa Shule ya Sekondari ya Bweni ya Mkwese inayomilikiwa na Jumuiya ya Wazazi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Manyoni mkoani Singida wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali waliohudhuria mahafali ya 42  yaliyofanyika jana shuleni hapo.

Wahitimu Wasichana wa Kidato cha  Nne wa Shule ya Sekondari ya Bweni ya Mkwese inayomilikiwa na Jumuiya ya Wazazi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Manyoni mkoani Singida wakiwa katika picha ya pamoja.

Wahitimu Wavulana wa Kidato cha  Nne wa Shule ya Sekondari ya Bweni ya Mkwese inayomilikiwa na Jumuiya ya Wazazi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Manyoni mkoani Singida wakiwa katika picha ya pamoja.

Mwekezaji wa Shule ya Sekondari ya Bweni ya Mkwese inayomilikiwa na Jumuiya ya Wazazi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Askofu Williams Yindi  akitoa dira ya shule hiyo katika mahafali ya 42 ya kidato cha Nne yaliyofanyika jana shuleni hapo wilayani Manyoni mkoani Singida.Mchungaji Robert Paul wa Kanisa ka Pentekoste la Kijiji cha Mkwese akiomba kabla ya kuanza mahafali hayo.
Burudani ikitolewa na wahitimu hao.
Mkuu wa Shule hiyo, Hamisi Yindi akizungumza katika mahafali hayo.
Wahitimu wakiwa kwenye mahafali hayo.
Wazazi, walezi, ndugu Jamaa na marafiki wa wahitimu hao wakiwa kwenye mahafali hayo.

Walimu wa shule  hiyo, wakiwa kwenye mahafali hayo. 
Wanafunzi wa kidato cha pili wakitoa burudani kwenye mahafali hayo.
Mahafali yakiendelea.
Viongozi wa dini wakiwa kwenye mahafali hayo.


Kaka Mkuu wa shule hiyo, Kelvine Alex (kushoto) na Dada Mkuu, Jacqueline Samson wakiwa kwenye mahafali hayo.
Wahitimu wakisoma risala. Kushoto ni Olivery Vedasto na Pili John.
Wahitimu hao wakionesha maonesho ya kisayansi jinsi ya kutumia adibini. Kutoka kushoto ni Elibariki Boniface, Grace Peter na Teryson Shillar.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya CCM Wilaya ya Manyoni,  Robert Chalamaganza, akizungumza  kwenye mahafali hayo.
Vyeti vikitolewa.

Mzee Romani Kanyaulega kutoka Dodoma akitoa nasaha kwa wahitimu hao.

Mama Joyce Kisuda, akitoa nasaha kwa wahitimu hao.Na Dotto Mwaibale, Manyoni.


SHULE ya Sekondari ya Bweni ya Mkwese inayomilikiwa na Jumuiya ya Wazazi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Manyoni mkoani Singida inatarajia kuanza kutoa  elimu ya stadi za ufundi ifikapo Januari 2021.

Hayo yalisema jana na Mwekezaji wa shule hiyo,  Askofu Williams Yindi wakati akitoa dira ya shule hiyo katika mahafali ya 42 ya kidato cha Nne tangu kuanzishwa kwake mwaka 1975 lakini tangu aanze kuiendesha yakiwa ni ya pili.

Alisema baada ya kufanya utafiti wa kutosha kwa kusoma nyakati amebaini kuwa wahitimu wa kidato cha nne cha sita na vyuo vikuu iwapo hawataweza kuyashika kwa akili zote yale wanayo fundishwa watajuta hasa katika kipindi hiki ambacho ni cha kizazi cha sayansi na teknolojia.

Alisema baada ya kufanya utafiti huo alibaini kuwa kuna mambo manne ambayo kijana aliyehitimu na kushindwa kuyashika vizuri masomo yake tangu mwanzo atakuwa katika changamoto kubwa katika safari yake ya maisha hivyo nguzo ya kwanza kwa vijana hao ni kuijua lugha ya kiingereza.

Alitaja nguzo ya pili ni kuwa vijana wapate elimu ya ufundi stadi kama uselemara, umeme, magari na kufundishwa stadi za michezo mbalimbali jambo litakalo saidia wahitimu hao wakiwa nyumbani kuwa na kitu cha kufanya baada ya kutoka shuleni.

Alisema tayari amekwisha wapata walimu wanne na januari mwakani wataanza rasmi kufundisha  masomo hayo.

Aliwataja walimu  ambao wataanza kufundisha kwa mkataba masomo hayo kuwa ni Mwalimu  Salum ambaye atafundisha lugha ya kiingereza ili wanafunzi hao waweze kuzungumza na kuandika, Mwalimu wa pili ni Gwamaka Chidodo ambaye ni mbobezi wa ufundi Selemara na watatu ni Mhandisi Godwin Gunda ambaye atafundisha ufundi magari na  Mwalimu wa nne ni Salumu Simba  yeye ni Mhandisi na mtaalamu wa masuala ya  umeme.

Yindi alisema  walimu hao ni wale waliostaafu toka serikalini na maeneo mengine na kuwa shule hiyo itaingia nao mkataba wa kufundisha shuleni hapo.

Alisema shule hiyo imejipanga vizuri kitaaluma kwani wanasafu nzuri ya walimu ambao wanapimwa kwa utendaji wao wa kazi ambapo aliwaondoa hofu wazazi na walezi  kutosita kuwapeleka watoto wao katika shule hiyo na wasitegemee kupokea vijana waliofeli.

Akizungumzia maendeleo ya shule hiyo tangu aanze kufanya uwekezaji alisema ameboresha miundombinu ya majengo, barabara, vyoo, madarasa, maji na umeme na kuwafanya wanafunzi kuzingatia masomo na kuacha kuomba udhuru wa mara kwa mara kutoka nje ya shule.

"Ninasimamia taaluma kwa kuliangalia kwa macho manne kama mtaendelea kuniletea vijana wenu hapa wategemee kupata daraja la kwanza, la pili na la tatu na si vinginevyo." alisema Yindi.

Wahitimu hao katika risala yao kwa mgeni rasmi ambaye alikuwa ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya CCM Wilaya ya Manyoni,  Robert Chalamaganza walisema  shule hiyo chini ya mwekezaji huyo imekuwa na maendeleo mazuri kitaaluma kwani ameweza kusimamia kikamilifu suala la elimu tofauti na miaka ya nyuma, wameweza kufanya mitihani mbalimbali ndani na nje ya shule ikiwa ni pamoja na mitihani ya utimilifu ya wilaya na kimkoa.

No comments:

Post a comment