Friday, 4 September 2020

WAZIRI ZUNGU AKIPONGEZA CHUO CHA UHASIBU ARUSHA


Na Zainab Nyamka,

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mussa Azzan Zungu amewapongeza Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA) kwa kuwa ni moja ya chuo kinachotoa wanafunzi bora kwa sasa.

Zungu amezungumza hayo wakati wa kutembelea maonesho ya Vyuo Vikuu yanayoendelea ndani ya Viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini.

Akitembelea banda la IAA, Zungu ameupongeza uongozi wa chuo hicho chini ya Prof Eliamani Sedokeya  Kwa kazi kubwa wanayoifanya ya kuhakikisha wanaendelea kutoa elimu bora kila mwaka.

Mbali na hilo, Chuo cha IAA kinaendelea na udahili wa wanafunzi wapya kwa ngazi ya Certificate, Diploma na Degree.

Afisa Uhusiano mwandamizi Sarah Goroi Amesema,  IAA ni chuo cha Serikali kilichopo chini ya Wizara ya Fedha na Mipango na kimekuwa ni moja ya Chuo kinachofanya vizuri na wanafunzi wanaotoka hapo wamekuwa wanafanya vizuri wanapopewa  nafasi za kazi.

Aisha, ameongeza kuwa katika maonesho haya ya Vyuo Vikuu wanaendelea na kudahili wanafunzi wapya kwa ngazi mbalimbali

Aidha Sarah amesema, muitikio wa wanafunzi ni mkubwa wakija kwa ajili ya kufanya udahili wa mwaka mpya wa masomo kwa ngazi tofauti zinazopatikana katika Chuo hicho.

Amesema, kwa mwaka huu wanadahili wanafunzi kwa kozi za Certificate in Insurance and Risk Management with Apprenticeship na Certificate in Bussiness Management With Chinese.

Kwa upande wa ngazi ya Diploma wana kozi za Diploma in Insurance and Risk Management with Apprenticeship, Diploma in Multimedia na Diploma in Bussiness Management With Chinese huku Kwa ngazi ya Bachelor Degree wana masomo ya Bachelor of Education with Computer Science, Bachelor  Of Econonic and Taxation, Bachelor with apprentiship, Bachelor of Accontancy with Information Technology  na Bachelor of  Insurance and Risk Management with Apprenticeship.

Aidha Sarah amewataka wanafunzi waendelee kujitokeza kwa wingi katika banda lao ili kufanya udahili pamoja na kupata ushauri mbalimbali wa masomo.
No comments:

Post a Comment