Wapongeza Wizara ya Madini kwa mabadiliko ya Sheria ya Madini_

Leo tarehe 25 Septemba, 2020 wadau mbalimbali wa madini kutoka katika mkoa wa Geita na mikoa ya jirani wamemiminika katika banda la Tume ya Madini kwenye Maonesho ya Teknolojia na Uwekezaji kwenye Sekta ya Madini yanayoendelea katika Uwanja wa Kituo cha Uwekezaji Bombambili Mkoani Geita.

Wakizungumza katika nyakati tofauti wamepongeza kazi inayofanywa na Wizara ya Madini na Tume ya Madini katika usimamizi makini wa Sekta ya Madini.

Wamesema mabadiliko makubwa ya Sheria ya Madini na kanuni zake yaliyofanywa na Wizara ya Madini yameleta mapinduzi makubwa kwenye Sekta ya Madini kwa kuwa manufaa ya dhahabu yameanza kuonekana katika mkoa wa Geita.

"Geita ya sasa imebadilika sio kama zamani, mji unakua kwa kasi sana kutokana na ongezeko la shughuli za uchimbaji na biashara ya madini," amesema Jackson Peter ambaye ni mchimbaji mdogo wa madini ya dhahabu katika mkoa wa Geita kwa niaba ya wadau wengine wa madini.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: