Meneja wa kanda ya kaskazini NEMC,Lweis Nzali akizungumza na waandishi wa habari Jana ofini kwake ,akiwataka kutumia vyombo vya habari kuelimisha wananchi juu ya matumizi ya mbinu mbalimbali za asili na za teknolojia rafiki za kuhifadhi mazingira


 Afisa mazingira NEMC, Josephati Antony akizungumza na waandishi wa habari akiwataka wananchi kulinda mazingira.
Sehemu ya waandishi wa habari
 

 Na Pamela Mollel, Arusha.

KUELEKEA kilele Cha maadhimisho ya siku ya Mazingira Duniani ambayo hufanyika Juni 5  ya kila mwaka wananchi wameshauriwa kulima kilimo cha matone badala ya kilimo cha mazoea ambacho kimekuwa kikiharibu mmomonyoko wa ardhi na kusabisha uharibifu wa mazingira

Hayo yameelezwa leo Juni 4,2020 na Meneja wa NEMC Kanda ya Kaskazini Lweis Nzali alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ambapo amewaomba kutumia vyombo vya habari kuelimisha wananchi kuhusu matumizi ya mbinu mbalimbali za asili na za teknolojia rafiki za kuhifadhi mazingira

Amesema kuwa siku ya mazingira kitaifa yalikuwa yafanyike mkoani Lindi lakini kutokana na  janga la ugonjwa wa Covid-19,imeamuriwa maadhimisho hayo kufanyika kwa kutumia vyombo vya habari pamoja na mitandao ya kijamii ili kuepuka mikusanyiko ya watu wengi ambayo inaweza kusabisha maambukizi ya virus hivyo.

Ameongeza kila mkoa utafanya maadhimisho kwa kutumia vyombo vya habari vilivyopo katika maeneo yao.Aidha amesema Tanzania inakabiliwa na changamoto kubwa ya uharibifu wa mazingira unaotokana na matumizi yasiyo endelevu ya rasilimali za kimazingira

Amezitaja changamoto hizo kuwa uharibifu wa ardhi,ufyekaji na uharibifu wa misitu, uharibifu wa vyanzo vya maji, uharibifu wa makazi ya viumbe wa majini na upotevu wa bioanuai

Kwa upande wake Ofisa Mazingira wa NEMC Josephati Antony amesema kuwa ili kulinda na kuhifadhi ikolojia ya mito,sheria ya mazingira ya mwaka 2004,sheria ya ardhi Namba 4 1999 , sheria ya mipango miji 2007,sheria ya usimamizi wa Rasilimali za maji 2009 zinazuia shughuli za binadamu eneo la hifadhi ya mita 60 ambalo linapimwa kutoka kingo za mito

Ameongeza kuwa  maeneo ya hifadhi ya mita 60 kutoka kwenye kingo za mito yana umuhimu mkubwa katika hifadhi ya maji na utoaji wa huduma ikolojia kwa binadamu yaani hewa Safi na makazi ya viumbe.Kauli mbiu ya mwaka huu inasema hivi "Tuhifadhi azingira kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi".
Share To:

Post A Comment: