Saturday, 27 June 2020

MADAKTARI WARIDHISHWA NA MAFUNZO WALIYOYAPATA KUTOKA WCF


 Daktari akionyesha stika atakayobandika kwenye hospitali anakotoka kuonyesha huduma za WCF zinapatikana kwenye hospitali husika, wakati wa kufungwa kwa mafunzo hayo
 Baadhi ya madaktari wakionyesha stika watakayobandikwa kwenye hospitali wanakotoka kuonyesha huduma za WCF zinapatikana kwenye hospitali hizo, wakati w akufungwa kwa mafunzo hayo
 Dkt. Nancy Shuma (kushoto) kwa niaba ya washiriki wenzake akikabidhiwa stika itakayobandikwa kwenye hospitali anayofanyia kazi kuonyesha huduma za WCF zinapatikana kwenye hospitali husika. Anayemkabidhi ni Mkuu w akitengo cha Mahusiano na Uhusiano wa umma WCF, Bi. Laura Kunenge.
 Dkt. Omar Chande (wapili kushoto), kwa niaba ya Mganga Mkuu wa Mkoa wa Arusha akikabidhio vyeti kwa washiriki.
 Dkt. Peter S. Mabula akizungumza kwa niaba ya washiriki wenzake wakati wa kufunga mafunzo hayo.
Dkt. Omar Chande, akitoa hotuba ya kufunga mafunzo kwaniaba ya mganga mkuu wa mkoa wa Arush
Mkurugenzi wa Huduma za Tiba na Tathmini wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Dkt. Abdulsalaam Omary
Dkt. Pascal M agesa, Afisa madai na tathmini WCF
Dkt. Ali Mtulia, Meneja anayeshughulikia madai na Tathmini WCF
Na
mwandishi wetu, Arusha-
MADAKTARI
waliokuwa wakishiriki mafunzo ya siku tano ya uelimishaji wa tathmini za
ulemavu utokanao na ajali na magonjwa yatokanayo na kazi kutoka mikoa ya Kanda
ya Kaskazini, wamefurahishwa na elimu waliyoipata na kwamba itasaidia kutenda
haki kwa pande zote mbili, wanufaika na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF).
Mafunzo
hayo yaliyoanza Juni 22, 2020 kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa (AICC)
jijini Arusha yaliandaliwa na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) ambapo zaidi
ya madaktari 100 kutoka mikoa ya Manyara, Arusha, Kilimanjaro na Tanga
walijifunza mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na Sheria iliyoanzisha Mfuko,
jinsi Mfanyakazi aliyeumia au kuugua kutokana na kazi anavyoweza kuwasilisha
madai, jinsi ya kufanya tathmini ya ulemavu uliotokana na ajali au ugonjwa
utokanao na kazi.
“Katika mafunzo haya
nipende kusema kwamba wakufunzi wamekuwa makini sana na wamefundisha kile
ambacho kilistahili na kila mmoja amekiri kuwa wakufunzi wamefanya kazi nzuri
na hata mazoezi ya vitendo kwa washiriki hakuna aliyepwaya.” Alisema Dkt. Peter
S. Mabula ambaye ni mwenyekiti wa washiriki.
Alisema
mafunzo hayo yamewaandaa kwenda kufanya kazi nzuri kuliko ile ambayo walikuwa
wakifanya hapo kabla.
“Mafunzo haya
yametuandaa kwenda kutenda haki kwa wagonjwa wetu na kwa Mfuko, wale wagonjwa
wanaokuja kwetu hatimaye wanakuja kupata fidia hivyo tumejifunza umakini wa
kufanya tathmini kwa umakini na ubora ili kutouibia mfuko au kumuibia
wateja  na hivyo sisi tunasimama katikati
ya wateja na mfuko ili tuweze kutenda haki.” Alisema Dkt. Mabula.
Akitoa
hotuba ya kufunga mafunzo hayo Dkt. Omar Chande kwa niaba ya mganga mkuu wa Mkoa
wa Arusha alipongeza hatua ya Mfuko kuongeza idadi ya wataalamu watakaoweza
kuwahudumia wagonjwa wanaohitaji kulipwa fidia.
“Fursa
hii ya utoaji mafunzo imekuja wakati muafaka na ni imani yangu kile
kilichofundishwa hapa ndicho kitakachokwenda kuondoa changamoto za watu ambao
hapo awali walipata shida inapofikia wakati wa kudai fidia.” Alisema Dkt.
Chande.
Naye
Mkurugenzi wa Huduma za Tiba na Tathmini wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi
(WCF), Dkt. Abdulsalaam Omary alisema mwaka 2015 Mfuko kupitia usaidizi wa
Shirika la Kazi Duniani uliweza kutoa mafunzo kama haya kwa madaktari 346 na
hadi kufikia Ijumaa Juni 26, 2020 madaktari wanaokaribia 1,000 tayari
wamepatiwa mafunzo.

No comments:

Post a Comment