Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.

Katika  kukabiliana na tatizo la fistula, Serikali kupitia Wizara ya
Afya,Maendeleo ya jamii,Jinsia ,Wazee na watoto  imetoa mafunzo juu ya
namna ya kutibu matatizo yatokanayo na uzazi na hasa namna ya
kumhudumia mama mjamzito mwenye uchungu pingamizi kwa watoa huduma za
Afya 676 katika Mikoa yote nchini.

Hayo yamebainishwa leo Bungeni Jijini Dodoma  kwa njia ya maandishi
kutoka Waziri Wa Afya, Maendeleo Ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
wakati ikijibu swali la  MHESHIMIWA SUSAN ANSELM  LYIMO Mbunge  (VITI
MAALUM) aliyehoji ,Tanzania ni moja ya nchi duniani zenye wagonjwa
wengi wa Fistula: Je Serikali imejipangaje  kupambana na ugonjwa wa
Fistula?

Katika Majibu kutoka Wizara ya Afya yamefafanua kuwa  Katika
kukabiliana na tatizo la fistula, Serikali kupitia Wizara ya
Afya,Maendeleo ya jamii,Jinsia ,Wazee na watoto  imetoa mafunzo juu ya
namna ya kutibu matatizo yatokanayo na uzazi na hasa namna ya
kumhudumia mama mjamzito mwenye uchungu pingamizi kwa watoa huduma za
Afya 676 katika Mikoa yote nchini.

Mikoa hiyo ni pamoja Mwanza, Kagera, Simiyu, Shinyanga, Kigoma, Kilimanjaro na
Dar es Salaam huku  Wizara ikitoa mafunzo maalum juu ya namna ya kufanya
upasuaji wa kurekebisha tatizo la fistula kwa madaktari 32 (Vesco and
Recto Vagina
Fistula Surgeons).


Hii imesaidia kupunguza matatizo mengine yanayotokana na fistula kama
vile unyanyapaa pamoja na sonona ambapo pia  ongezeko la vituo vya
afya vilivyoboreshwa na mwamko wa kina mama kwenda kliniki na
kujifungua kwenye vituo vya afya vimesaidia kupunguza sana tatizo  la
fistula nchini.

 Ikumbukwe kuwa fistula ni shimo ambalo hutokea kati ya kibofu cha mkojo na
sehemu ya siri   au katikati ya njia ya haja kubwa  kwa mwanamke
ambaye amejifungua kwa shida ya uchungu pingamizi na Shimo hutokea
pale ambapo kichwa cha mtoto ni kikubwa kuliko njia ya uzazi ambapo
Fistula inasababishwa na kusukuma mtoto wakati wa kujifungua kwa muda
mrefu bila usaidizi au matibabu yeyote, na anachanika katika njia ya
uzazi na kusababisha shimo, hivyo husababisha uvujaji wa haja kubwa au
mkojo bila kujizuia huku ikielezwa kuwa  kujifungua mapema kabla ya
umri kumekuwa chanzo kikubwa cha kutokea fistula.
Share To:

Post A Comment: