Na Esther Macha, Mbeya
MSHIRIKA mwenza kiongozi katika ofisi ya uwakili Baki Mwabukusi and Chamber Advocate iliyopo eneo la forest ya zamani ,Boniface Mwabukusi amesema kuwa wakulima wa chai  na  Kakao Wilayani Busokelo Mkoani Mbeya wamekuwa wamekuwa hawatendewi haki  licha ya kuwa mazao hayo ni ya  kimkakati katika kumkomboa  wakulima .
Alisema  hayo jana wakati akizungumza na Mtandao huu ofisini kwake kuhusiana na changamoto ambazo  wakulima  wamekuwa wakikumbana nazo katika harakati za kuhakikisha wanajikomboa kiuchumi
Mwabukusi alisema kwamba jambo lingine ni kwamba hakuna jitihada zozote zinazoeleweka ambazo zimewekwa katika kutafuta masoko yenye tija katika uzalishaji kwa mkulima.
Hata hivyo Mwabukusi alisema kuwa wakulima wa zao la chai bado hawatendewi haki ,lakin bado wakulima wa kakao bado wameachwa nyuma
“Mkulima huyu anahitaji kusaidiwa ili aweze kujikomboa kiuchumi hivyo ni muhimu awe na uhakika wa kupata masoko yenye tija kwake ambayo yatamfanya kuuza mazao yake kwa nafasi na kujipatia kipato ambacho kitamwezesha kumudu kuendesha maisha yake”alisema Mwanasheria huyo .
Aidha aliongeza kuwa zao la viazi mvilingo hakuna jitihada zozote ambazo zimewekwa za kumsaidia mkulima katika kutafuta masoko yenye tija ,kukosekana kwa mpango madhubuti wa thamani wa mazao jambo ambalo linapekelekea wakulima kufilisika kutokana na kukopa kwenye taasisi za kibenki.
Aliongeza kuwa jambo lingine ni ufugaji ambapo kumekuwa na hali ya kumkandamiza mfugaji wa ng,ombe wa maziwa jambo ambalo linasababisha kushindwa kufanya kazi zao kwa ushindani wa haki .
Share To:

Post A Comment: