Mbunge wa Isimani Mhe Wiliam Lukuvi
Mbunge wa jimbo la Isimani Mhe Wiliam Lukuvi amesema zoezi la ufungaji TV katika vijiji vya jimbo hilo ni mpango wa serikali wa kuwezesha wananchi kupata taarifa mbali mbali .
Alisema serikali toka mwaka jana ilianza kutoa dishi na ving'amuzi wakati kwa upande wake kama Mbunge alichangia TV ili wananchi waweze kufikiwa na mpango wa elimu kwa umma kwa kuwafanya wananchi hasa wa vijijini wasio na uwezo wa kununua TV kila mmoja aweze kupata elimu hiyo . " Niliomba UCAF kama wabia wa serikali wakanipatia ving'amuzi na madish na mimi nikanunua TV ili kufunga kwenye maeneo ambayo wananchi wameyaandaa na kuyawekea umeme kwa gharama zao kwenye vijiji vyote vya jimbo la Ismani"
Lengo ni kuwahabarisha wananchi juu ya utekelezaji wa ilani ya CCM ngazi ya kitaifa, Kusikiliza hotuba mbali mbali za viongozi wa kitaifa, kuhabarika na kupata elimu ya matukio mbalimbali ya kitaifa na kimataifa" zihusuzo afya,kilimo, elimu,ufugaji,uvuvi,hali ya hewa, michezo alisema Lukuvi .
Pia alisema kuwa kwenye mkutano mkuu wa jimbo wananchi uliofanyika mwaka jana wananchi waliomba zoezi la kusambaza TV hizo kuendelea kutolewa zaidi ili wote waweze kufuatilia vipindi vya elimu kwa umma kupitia TV .
Post A Comment: